RIP! Mchekeshaji Fred Omondi amefariki

Omondi alikuwa akiendelea kuhudumiwa katika Hospitali ya Mama Lucy wakati alipokata roho.

Muhtasari

•Mtumbuizaji huyo ambaye ni kaka mdogo Eric Omondi alikuwa akiendelea kuhudumiwa katika Hospitali ya Mama Lucy wakati alipokata roho.

Image: INSTAGRAM// FRED OMONDI

Mchekeshaji Fred Omondi amefariki dunia.

Mtumbuizaji huyo ambaye ni kaka mdogo Eric Omondi alikuwa akiendelea kuhudumiwa katika Hospitali ya Mama Lucy wakati alipokata roho.

Maelezo kuhusu kilichosababisha kifo chake bado hayajabainika wazi lakini duru za kuaminika zinaarifu kwamba alihusika katika ajali ya barabarani

Habari za kifo chake zilithibitishwa na mchekeshaji na mtayarishaji wa maudhui Terence Creative ambaye alisema aliaga Jumamosi mwendo wa asubuhi.

“LEO SAA KUMI NA MBILI KAMILI ASUBUHI NIMEPOKEA SIMU YA KUSIKITISHA KULIKO ZOTE 💔🖤 Inauma...... Fred namshukuru Mungu kwa muda aliotupa pamoja kaka, umekuwa sehemu ya kazi yangu na ukuaji wa tasnia, wewe daima. Alinichukulia kama kaka na kunikaribisha nilipokuwa sina pa kwenda, alinipa jukwaa na kunilipa, pamoja tulianza shoo ya vichekesho vya klabu, nitathamini sana wakati tuliposhiriki jukwaa pamoja kutoka Tribeka, Taj Mall, Hearts, i club etc hadi tulipofika kwenye show ya Churchill na kisha kuandaa kipindi chetu cha kwanza cha Tv pamoja: Ktn Crazy Comedy.

"Pamoja tuliteseka, kwa pamoja tulijifunza na kwa pamoja tulitia moyo, tulifanya watu wacheke na kuunda kumbukumbu kubwa. Haya yote nitayathamini na kuyashika sana, Freddy ulikuwa mwanaume, nina mengi ya kusema juu yako lakini yote naweza kusema." bro ni kwamba ulifanya vizuri na utakumbukwa na kukosa, Nenda vizuri kaka," Terence aliomboleza.

Leo, Fred alikuwa amepanga kutumia wikendi yake katika mji wa Meru kama ilivyoshirikiwa kwenye Instastori zake..