Hakuna ushahidi! Jacque Maribe aondolewa mashtaka ya mauaji ya Monica Kimani

Maribe aliondolewa mashtaka na Jaji Grace Nzioka wa Mahakama ya Milimani mnamo Ijumaa, kwa kukosa ushahidi.

Muhtasari

•Mwanahabari Jacque Maribe ameondolewa mashtaka katika kesi ya mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani.

akiwa katika Mahakama ya Milimani, mbele ya Hakimu Grace Nzioka mnamo Februari 9, 2024, wakati wa hukumu ya kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani .
Jackie Maribe akiwa katika Mahakama ya Milimani, mbele ya Hakimu Grace Nzioka mnamo Februari 9, 2024, wakati wa hukumu ya kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani .
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mwanahabari Jacque Maribe ameachiliwa huru katika kesi ya mauaji ya Monica Kimani.

Maribe aliachiliwa na Jaji Grace Nzioka wa Mahakama ya Milimani mnamo Ijumaa, kwa kukosa ushahidi.

Yeye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ambayo imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya miaka mitano.

Kulingana na Jaji Nzioka, shtaka lililotolewa dhidi ya Maribe halikuwekwa ipasavyo.

"Ni maoni yangu kwamba shtaka lililoletwa dhidi ya mshtakiwa wa pili halikuwa shtaka sahihi," alisema.

"Je, kulikuwa na kosa lolote wakati mshtakiwa wa pili alipotoa taarifa kwa afisa wa upelelezi katika kituo cha polisi cha Lang'ata ambayo ilibainika kuwa si kweli? Sisemi tena. Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma inajua wajibu wao.