Covid-19: 18 waaga dunia, visa 486 vipya vyaripotiwa

Hii leo, visa 486 vipya  vimeripotiwa humu nchini kutokana na sampuli 4,134 zilizopimwa katika masaa 24 yaliyopita.

Kutokana na visa hivyo vipya, 463 ni wakenya huku 23 wakiwa wageni. 278 ni wanaume  na 208 ni wanawake.

Mgonjwa mchanga zaidi ana umri wa miezi mitatu huku mkongwe zaidi akiwa na miaka 94.

Kufikia sasa idadi ya visa vilivyoripotiwa nchini vimefikia 145,670 huku sampuli zilizopimwa zikifikia 1,561,838.

Katika habari za kutia moyo ni kuwa watu 490 wamepata nafuu kutokana na virusi hivyo, 318 kutoka vituo mbalimbali vya afya humu nchini na 172 wakiwa manyumbani mwao.

Idadi ya wagonjwa waliopata nafuu imefika 99,095.

Katika habari za kuvunja moyo ni kuwa vifo 18 vimeripotiwa katika masaa 24 yaliyopita huku wawili hao wakiaga katika masaa 24 yaliyopita.

Idadi ya watu walioaga dunia kutokana na Covid-19 sasa imefikia 2,348.