Naibu rais William Ruto aeleza makosa ya uongozi wa Uhuru Kenyatta

Rais Kenyatta alipuuza ushauri wa Ruto kuweka wazi kandarasi za mikopo baina ya Kenya na Uchina.

Muhtasari

•Naibu rais siku ya Jumanne alidai kwamba rais Kenyatta alipuuza ushauri wake kuweka wazi kandarasi za mikopo baina ya Kenya na Uchina.

WILLIAM WANYOIKE
WILLIAM WANYOIKE

Naibu rais alitoa madai kuwa utovu wa usalama na mauaji yanayoshuhudiwa katika maeneo ya Kerio Valley yamechochewa kisiasa ili kuadhibu wafuasi wake.

Akizungumza Jumanne usiku katika mdahalo wa urais naibu rais pia alidai kuwa serikali ya Uhuru Kenyatta imesababisha kudidimia kwa sekta ya kilimo kutokana na  kuongezeka kwa pembejeo.