Wafahamu Makatibu wa Kudumu wanawake katika serikali ya Ruto

Teresia Mbaika Malokwe, Esther Ngero na Aurelia Rono ni baadhi tu ya waliopendekezwa.

Muhtasari

•Rais William Ruto aliwapendekeza zaidi ya wanawake kumi kuwa Makatibu wa kudumu katika idara mbali mbali za serikali.

Makatibu wa Kudumu Wanawake katika serikali ya Rais William Ruto.
Image: RADIO JAMBO

Siku ya Jumatano, rais William Ruto aliwapendekeza zaidi ya wanawake kumi kuwa Makatibu wa kudumu katika idara mbali mbali za serikali.

Baadhi ya wanawake hao ni kama; Teresia Mbaika Malokwe wa Idara ya Ugatuzi, Esther Ngero  Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji na Aurelia Rono wa Idara Masuala ya Bunge.

Wengine ni Caroline Nyawira Murage wa Idara ya Huduma za magereza, Beatrice Inyangala Elimu ya Juu na Utafiti, Roseline Njogu wa Masuala ya Ughaibuni na Veronica Nduva Jinsia na usawa.

Josephine Mburu wa Idara ya Ubora na usimamizi wa Afya, Esther Thaara Muhoria wa Idara ya  TVET na Susan Mangeni MSMEs