Mfahamu mwanadada aliyekufa maji na mpenziwe Juja

Bi Fridah alizikwa siku ya Jumatano katika eneo la Mathioya, kaunti ya Muranga.

Muhtasari

•Kamuyu, 23, alifariki baada ya gari alilokuwa ndani yake kutumbukia kwenye bwawa moja katika eneo la Titanic mnamo Januari 17.

Mfahamu mwanadada aliyekufa maji na mpenziwe Juja
Image: WILLIAM WANYOIKE

Fridah Warau Kamuyu, mwanamke aliyekufa maji kwenye bwawa la Juja, Kaunti ya Kiambu, akiwa na rafiki yake wa kiume hatimaye alizikwa siku ya Jumatano.

Kamuyu, 23, alifariki baada ya gari alilokuwa ndani yake pamoja na mfanyibiashara wa Kiambu, Titus Kiiru mwenye umri wa miaka 39, kutumbukia kwenye bwawa moja katika eneo la Titanic mnamo Januari 17.