Hujuma! Harmonize alalamikia dhulma katika muziki

Harmonize alisema yuko tayari kufa akipigania haki zake na wenzake.

Muhtasari

•Harmonize alifunguka kuhusu baadhi ya dhuluma ambazo yeye na baadhi ya wasanii wenzake wengine wamekuwa wakipitia katika tasnia ya muziki.

Harmonize alalamikia dhulma katika muziki
Image: ROSA MUMANYI

Siku ya Jumanne, staa wa bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize alifunguka kuhusu baadhi ya dhuluma ambazo yeye na baadhi ya wasanii wenzake wengine wamekuwa wakipitia katika tasnia ya muziki.

Ingawa hakumtaja mkandamizaji wake, bosi huyo wa Kondegang alionekana kumlenga bosi wake wa zamani na kampuni ya kusambaza muziki wake. Alisema kuwa amenyanyaswa na kudhulumiwa kwa sana.

Harmonize alisema yuko tayari kufa akipigania haki zake pamoja na wasanii wenzake mradi awe ameacha utajiri mkubwa kwa binti yake.

Baadhi ya madai ambayo aliibua ni pamoja na:-

  • Sijapokea hela za uchapishaji muziki kwa miaka 7
  • Kuna mtu anadai kumiliki miziki yangu inapochapishwa.
  • Kunyanyaswa na kudhalilishwa sana.
  • Nitakata ushirikiano na Mziiki nisipoelezwa ukweli.
  • Wazalishaji wamenyimwa haki ya kuchapisha ngoma.
  • Siogopi mtu mwingine ila Mungu na serikali
  • Nitafurahi nikifa leo na nimuache binti yangu tajiri
  • Ninapigania wasanii wengi wanaodhulumiwa.