Orodha ya mambo ya kutatanisha yaliyofanywa na Eric Omondi kwa jina la uanaharakati

Mwaka jana mchekeshaji huyo aliandamana nusu uchi jijini Nairobi.

Muhtasari

•Jumanne, Eric Omondi  alisababisha msongamano wa magari katika barabara ya Lang’ata jijini Nairobi baada ya kufunga njia hiyo yenye shughuli nyingi ili kusambaza unga kwa wakazi.

•Mwezi uliopita, mchekeshaji huyo aliongoza kundi la waandamanaji kulalia magodoro kwenye barabara ya Jomo Kenyatta jijini Kisumu.

Mambo ya kutatanisha yaliyofanywa na mwanaharakati Eric Omondi
Image: HILLARY BETT

Siku ya Jumanne, mchekeshaji Eric Omondi  alisababisha msongamano wa magari katika barabara ya Lang’ata jijini Nairobi baada ya kufunga njia hiyo yenye shughuli nyingi ili kusambaza unga kwa wakazi.

Mchekeshaji huyo mwenye utata mwingi aliyebadilika kuwa mwanaharakati alichukua hatua hiyo kama njia ya kupigana na gharama ya juu ya maisha. Wakazi walijitokeza kwa wingi kupata unga huku akizozana na madereva.

Tukio la  siku ya Jumanne sio jambo la kwanza lenye utata kwa mchekeshaji huyo kufanya kwa jina la uanaharakati.

Katika grafiki ya leo. tunaangazia mambo mengine ya kustaajabisha ambayo aliwahi kufanya hapo awali.