Fahamu maeneo ambayo mastaa wa Kenya walienda honeymoon baada ya harusi

Mwaka wa 2015, wanahabari Betty Kyallo na Dennis Okari walifurahia fungate nchini Mauritius na Dubai.

Muhtasari

•Akothee anaendelea kufurahia fungate (honeymoon) na mume wake Denis Shweizer almaarufu Omosh jijini Santorini, Ugiriki.

ambayo mastaa wa Kenya walienda honeymoon baada ya harusi.
Maeneo ambayo mastaa wa Kenya walienda honeymoon baada ya harusi.
Image: ROSA MUMANYI

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee anaendelea kufurahia fungate (honeymoon) na mume wake Denis Shweizer almaarufu Omosh jijini Santorini, Ugiriki.

Wawili hao walifunga ndoa katika harusi ya kufana mnamo Aprili 10 baada ya kuchumbiana kwa miezi kadhaa.

Wanandoa hao ni miongoni mwa watu mashuhuri wa Kenya waliofanya fungate katika maeneo mazuri sana katika siku za hivi majuzi.

Wengine ni pamoja na;

  • Akothee na Denis Shweizer – Santorini, Greece (2023) 
  • Kamene Goro na Deejay Bonez – Elementaita (2023)
  • Catherine Kamau na Philip Karanja – Sychelles (2017)
  • Dennis Okari na Betty Kyallo (walitengana) – Mauritius & Dubai (2015)
  • Juliani na Lilian Ng’aang’a – Meru (2022)
  • Gloria Muliro na Evans Sabwami – New York, USA (2021)
  • Moji Shortbabaa na Nyawira Gachugi – Elementaita (2021)
  • Lucy Natasha na Prophet Carmel – Diani, Kwale (2022)