Matetemeko ya ardhi mabaya zaidi kutokea katika miongo miwili iliyopita

Siku ya Ijumaa, nchi ya Morocco ilikumwa na tetemeko mbaya la ardhi lililoua zaidi ya watu 2200.

Muhtasari

•Zaidi ya watu 300,000 katika eneo la Marrakesh, Morocco na viunga vyake wameathiriwa na janga hilo. 

•Katika grafiki ya leo, tunaangazia mataifa mengine ambayo yamekumbwa na mitetemeko mibaya ya ardhi katika miaka ya hivi majuzi.

mabaya zaidi katika miongo miwili iliyopita (2003-2023)
Matetemeko ya ardhi mabaya zaidi katika miongo miwili iliyopita (2003-2023)
Image: HILLARY BETT
mabaya zaidi katika miongo miwili iliyopita (2003-2023)
Matetemeko ya ardhi mabaya zaidi katika miongo miwili iliyopita (2003-2023)
Image: HILLARY BETT

Siku ya Ijumaa, nchi ya Morocco ilikumwa na tetemeko mbaya la ardhi la kipimo cha 6.8. Zaidi ya watu 300,000 katika eneo la Marrakesh na viunga vyake wameathiriwa na janga hilo. 

Waokoaji bado wanahangaika kuokoa familia nzima zilizokwama chini ya vifusi vya majengo yaliyoanguka, haswa katika vijiji. Zaidi ya watu 2,000 wamejeruhiwa - zaidi ya 1,400 wakiwa wamejeruhiwa vibaya Kwa kuhofia mitetemeko ya baadaye, wenyeji katika jiji kuu la kusini la Marrakesh pia walilala nje mahali pa wazi jana usiku.

Katika grafiki ya leo, tunaangazia mataifa mengine ambayo yamekumbwa na mitetemeko mibaya ya ardhi katika miaka ya hivi majuzi.