Magavana waliookolewa na seneti baada kubanduliwa na MCAs

Tangu ujio wa ugatuzi mwaka 2013, magavana kadhaa wamejipata katika hali ngumu ya kujitetea mbele ya seneti baada ya MCAs wa kaunti zao kupitisha hoja ya kuwabandua.

Muhtasari

• Katika miswada yote ambayo imewahi kuidhinishwa na MCAs, miwili tu ndio ilifanikiwa kuwabandua magavana ofisini.

• Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu na mwenzake wa Nairobi kipindi hicho Mike Sonko waliangukiwa na shoka la kubanduliwa.