Wafahamu wanasoka wa Afrika waliozirai uwanjani na kufariki

Raphael Dwamena wa Ghana alifariki siku ya Jumamosi baada ya kuzimia wakati akicheza nchini Albania.

Muhtasari

•Dwamena, 28, alifariki nchini Albania baada ya kuzimia uwanjani wakati kwa mchuano baina ya klabu yake ya KF Egnatia na Partizani.

wa Afrika waliozirai uwanjani na kufariki.
Wanasoka wa Afrika waliozirai uwanjani na kufariki.
Image: HILLARY BETT

Waghana wanaomboleza kifo cha mmoja wa washambuliaji bora kuwakilisha taifa hilo katika mashindano ya kimataifa, Raphael Dwamena aliyekata roho siku ya Jumamosi.

Dwamena, 28, anaripotiwa kufariki dunia nchini Albania baada ya kuzimia uwanjani wakati kwa mchuano baina ya klabu yake ya KF Egnatia na Partizani siku ya Jumamosi.

Ripoti zinaashiria kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Levante alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa anacheza uwanjani, hali iliyopelekea kifo chake cha ghafla.