Wafahamu maafisa wa serikali ambao mkuu wa utumishi wa umma anataka wafutwe

Alhamisi, mkuu wa Utumishi wa Umma, Felix Koskei anataka maafisa 74 kusimamishwa kazi kwa tuhuma za ufisadi.

Muhtasari

•Mkuu wa Utumishi wa Umma, Felix Koskei ameagiza kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi sita, mhasibu mmoja na maafisa 67 wa polisi kwa madai ya ufisadi.

ambao mkuu wa utumishi wa umma anataka wafutwe kazi.
Maafisa wa serikali ambao mkuu wa utumishi wa umma anataka wafutwe kazi.

Siku ya Alhamisi, mkuu wa Utumishi wa Umma, Felix Koskei anataka maafisa 74 kusimamishwa kazi kwa tuhuma za ufisadi.

74 hao ni pamoja na:-

  • Fredrick Mwamati, Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Maendeleo ya Maji ya Tanathi.
  • Stephen Ogenga, Mkurugenzi Mkuu wa NITA.
  • Stanvas Ong’alo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya.
  • Benjamin Kai Chilumo, Mkurugenzi Mtendaji wa Sekretarieti ya Huduma Center.
  • Peter Gitaa Koria, Mkurugenzi Mtendaji wa Bomas of Kenya.
  • Anthony Wamukota, Meneja Mkuu wa KETRACO.
  • Esther Wanjiru Chege, Mhasibu wa KeRRA.
  • Maafisa 67 wa polisi.