Fahamu kikosi kilicho nyuma ya mafanikio ya Diamond Platnumz

Diamond ameorodheshwa miongoni mwa wanamuziki matajiri, wenye bidii na maarufu zaidi.

Muhtasari

•Diamond sio tu mwanamuziki mahiri bali pia ameorodheshwa miongoni mwa wanamuziki matajiri zaidi, wenye bidii na maarufu.

Kikosi nyuma ya mafanikio ya Diamond Platnumz
Image: HILLARY BETT

Bila shaka bosi wa WCB Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii waliofanikiwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kote Afrika.

Diamond sio tu mwanamuziki mahiri bali pia ameorodheshwa miongoni mwa wanamuziki matajiri zaidi, wenye bidii na maarufu.

Ingawa ametia bidii kubwa kujizolea mafanikio yake makubwa, hayajakuja kwa juhudi zake pekee yake. Kumekuwa na timu ya watu kadhaa ambao wametoa michango mbalimbali katika mafanikio ya staa huyo wa Bongo.

Mameneja Babu Tale, Mkubwa Fella, Don Fumbwe na miongoni mwa watu ambao wamesaidia kumuinua mwimbaji huyo. Wengine ni pamoja na mama yake Mama Dangote, Wazalishaji S2Kizzy na Hanscana, mcheza santuri Rommy Jons, wandani wake Baba Levo na Mbosso na wasaidizi wengine kadhaa.