Siasa na Injili: Wafahamu wainjilisti wanaoshiriki siasa nchini Kenya

Gavana wa Meru, Kawira Mwangaza ni Askofu katika Kanisa la Baite Family Fellowship.

Muhtasari

•Baadhi wa wanasiasa mahiri wa Kenya wanahudumu katika tasnia ya injili kwa njia moja au nyingine.

Image: ROSA MUMANYI

Baadhi wa wanasiasa mahiri wa Kenya wanahudumu katika tasnia ya injili kwa njia moja au nyingine.

Gavana wa Meru, Kawira Mwangaza pia ni Askofu katika Kanisa la Baite Family Fellowship, mjini Meru.

Aliyekuwa mgombea Useneta wa Nairobi kwa tiketi ya UDA, Margaret Wanjiru ni Askofu katika kanisa la Jesus is Alive Ministries.