logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jinsi Kongamano la Wanaume la Kenya lilivyofanyika (+Picha)

Hafla hiyo ilianza saa nane mchana na kuendelea hadi baadaye jioni.

image
na SAMUEL MAINA

Habari15 February 2023 - 07:31

Muhtasari


  • •Hafla hiyo iliyofanyika katika Carnivore Simba Saloon ilianza saa nane mchana na kuendelea hadi baadaye jioni.
  • •Wanajopo walijumuisha aliyekuwa Jaji Ian Mbugua, wakili Danstan Omari, Dkt Frank Njenga, Mjumbe Robert Alai, Mhubiri Simon Mbevi na Chris Kirwa.
wakiwasili kwenye Carnivore Simba Saloon kwa ajili ya Kongamano la Wanaume 2023 siku ya Jumanne Februari 14.

Kongamano halisi la kwanza kabisa la Wanaume kutokea nchini Kenya lilifanyika katika Carnivore Simba Saloon siku ya Jumanne alasiri.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Kongamano la Wanaume wa Kujitangaza Stephen Letoo ilianza saa nane mchana na kuendelea hadi baadaye jioni.

Wanaume wa rika tofauti kutoka sehemu mbalimbali za nchi walihudhuria hafla hiyo iliyopambwa na watu kadhaa mashuhuri nchini.

Mfawidhi wa tukio hilo lenye utata alikuwa mchekeshaji Dr Ofweneke pamoja na mtangazaji maarufu Shaffie Weru.

Wanajopo wa Toleo la Kenya la Kongamano la Wanaume la 2023 walijumuisha aliyekuwa Jaji wa Tusker Project Fame Ian Mbugua, wakili maarufu Danstan Omari, Mwanasaikolojia Dkt Frank Njenga, Mjumbe wa Kileleshwa Robert Alai, Mhubiri Simon Mbevi na Chris Kirwa.

Wageni wengine ni pamoja na mwanahabari mkongwe Swaleh Mdoe, kiongozi wa Wachache katika Kaunti ya Nairobi Mhe. Anthony Kiragu Karanja miongoni mwa wengine.

Miongoni mwa mada za siku hiyo ni Afya ya Akili ya Wanaume, Ndoa za wake wengi, Mahusiano, Masuala ya Uzazi Wenza, Talaka na Uzazi.

Tazama Picha la Hafla hiyo:-


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved