Kenya yamfurusha Mzambia kwa madai ya uuzaji wa dhahabu feki na ulaghai wa pesa

Waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i alitoa maagizo ya kurejeshwa kwa mshukiwa kwao

Muhtasari

•Raia wa Zambia anayeshutumiwa kwa kuendesha kundi la kimataifa la walaghai wa dhahabu na sarafu bandia jijini Nairobi, amerejeshwa kwao.

•Kulingana na polisi, Bupe Chipando, almaarufu Elena, alikamatwa na wapelelezi baada ya kudaiwa kulaghai Raia wa Uholanzi zaidi ya Ksh.170 milioni katika mkataba wa dhahabu ghushi.

Kenya Yamfukuza Mzambia Mshukiwa wa Dhahabu Feki, Ulaghai wa Pesa
Kenya Yamfukuza Mzambia Mshukiwa wa Dhahabu Feki, Ulaghai wa Pesa
Image: DCI

Raia wa Zambia anayeshutumiwa kwa kuongoza kundi la kimataifa la walaghai wa dhahabu na sarafu bandia jijini Nairobi, amerejeshwa kwao.

Kulingana na polisi, Bupe Chipando, almaarufu Elena, alikamatwa na wapelelezi baada ya kudaiwa kulaghai Raia wa Uholanzi zaidi ya Ksh.170 milioni katika mkataba ghushi wa biashara ya dhahabu.

Awali Bw. Chipando pia alikuwa amehusishwa na uchapishaji wa fedha ghushi.

Waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i alitoa maagizo ya kurejeshwa kwa mshukiwa aliyesafirishwa  kutoka hapa nchini dakika chache kabla ya saa sita usiku.

"Bupe, ambaye pia alihusika katika uchapishaji wa sarafu ghushi, alirejeshwa kwao nyumbani saa 1145 leo, kufuatia maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt Fred Matiang'i," Kurugenzi ya Uchunguzi wa Jinai ilisema Jumapili, Julai 10.

Kufukuzwa kwake yanajiri mwezi mmoja baada ya mwanamume mmoja wa Sudan anayesemekana kuwa "mkimbizi wa kimataifa" kufukuzwa katika maficho yake katika makao ya wafanyikazi wa Chuo Kikuu cha Nairobi.

Wapelelezi mnamo Juni 7 walisema wamebaini kuwa Mohamed Nagi Mohamed Magzoub, ambaye alikuwa na hati ya kusafiria ya Sudan, anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kupangwa nchini humo.

Wakati huo, serikali ilisema mipango ya kumrejesha mshukiwa huyo Khartoum ilikuwa inaendelea.