- Trump amesema hali yake imeboreka ingawaje haijulikanai iwapo amepona
- Rais huyo amekuwa akitibiwa katika hospitali moja ya kijeshi
Mgombeaji wa rais wa marekani wa tiketi ya chama cha democrat Joe Biden amesema hapafai kuwa na awmau ya pili ya mdahjalo wa urais iwapo rais Donald Trum bado hajapona virusi vya corona .
" Nafikiri bado anaugua covid 19 ,hatufai kuwa na mjadala huo’ Biden amesema siku ya jumanne
" Nafikiri itatulazimu kufuata kanuni kali .watu wengi wameambukizwa na hili ni tatizo kubw’
Mjadala huo wa wagombeaji wa urais ulifaa kufanyika oktoba tarehe 15 Miami Florida
Trump alipatikana na virusi vya corona tarehe 1 oktoba lakini haijulikani aliambukizwa lini ugonjwa huo
Kulingana na mwongozo wa kiafya nchini Marekani Trump anafaa kujitenga kwa siku 10 tangu siku anayoaanza kuona daalili za ugonjwa huo . Matamshi ya Biden yanajiri baada ya kuibuka ripoti kwamba ugonjwa huo unasambaa kwa haraka miongoni mwa watu wanaokaribiana na Trump huku afisa moja wa kijeshi akiambukizwa pamoja na mshauri wa rais Stephen Miller .
Bwana Miller, ambaye amejitenga kwa siku tano sasa amethibitisha kwamba aliambukizwa virusi hivyo siku ya jumanne .
Jenerali mmoja wa kijeshi Mark Milley na viongozi wengine wa jeshi pia wapo katika karantini baada ya afisa wa kikosi cha ulinzi cha Coast Guard Admiral Charles Ray kupatikana na virusi hivyo .