- Rais Trump na mkewe ni miongoni mwa walioambukizwa corona lakini sasa wamepona
- Maafisa wengine wa White House pia walipatwa na maradhi hayo
Mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump Barron ,mwenye umri wa miaka 14 aliambukziwa virusi vya corona lakini sasa amepona ,amesema mke wa rais Melania Trump
Melania alisema hofu yake iligeuka kuwa ukweli wakati Barron alipopatiukana na virusi hivyo lakini amesema kwa bahati nzuri ‘ni kijana mwenye nguvu ‘ na hakuonyesha daalili zozote .
Rais Trump na Melania walipatikana na virusi hivyo pamoja na wafanyikazi wengine wa White House lakini wamepona . Trump pia alithibitisha kwamba mwanawe alikuwa na corona kwa kusema kwamba ‘ alikuwa na ugonjwa huo kwa muda mfupi’ wakati wa mkutano wa kampeini katika jimbo la Iowa .
Kura za maono zaonyesha kwamba Trump yupo nyuma ya mpinzani wake Joe Biden huku zikisalia wiki tatu tu kabla ya uchaguyzi wa Novemba tarehe 3 lakini ushindani kato yao umejibana sana katika majimbo mengi muhimu
Bwana Boden hakuwa na mikutano ya kampeini siku ya jumatano lakii alifanya hafla ya mchango kupitia njia ya mtandao na kutuma ujumbe uliorekodiwa kwa shirika la waislamu nchini marekani . Mrengo wa Biden ulitangaza kwamba ulipata mchango wa dola milioni 294 mwezi septemba .