Kwa nini waandamanaji wa Nigeria wanamtaka Beyoncé kuwa kama Rihanna

Muhtasari

• Rihanna, Kanye West na Nicki Minaj ni miongoni mwa watu mashuhuri waliojitokeza kuunga mkono maandamano dhidi ya ukatili wa polisi.

• Rihanna aliweka kwenye mtandao wake wa Twitter picha ya bendera ya Nigeria

Awali waandamanaji walitaka kuvunjiliwa mbali wa kitengo maalum cha polisi wakukabiliana na wizi wa kimabavu (Sars). Picha: REUTERS
Awali waandamanaji walitaka kuvunjiliwa mbali wa kitengo maalum cha polisi wakukabiliana na wizi wa kimabavu (Sars). Picha: REUTERS

Rihanna, Kanye West na Nicki Minaj ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamejitokeza kuunga mkono maandamano dhidi ya ukatili wa polisi nchini Nigeria. Lakini waandamanaji walimkaripia Beyoncé alipozungumzia suala hilo. Kwanini?

Waandamanaji usiku ya Jumanne mjini Lagos walisema wanaume waliokuwa wamevalia sare za polisi waliwafuata na kuanza kuwapiga risasi walipokuwa wanaimba wimbo wa taifa, madai ambayo wanajeshi wanapinga wakisema ni "taarifa ghushi".

Hatua iliyozua gumzo kali kote duniani. Mchekeshaji wa Afrika Kusini Trevor Noah alisema: "Kama tulivyoshuhudia nchini Marekani, polisi wa Nigeria wanavunja maandamano y akupinga ukatili wa polisi kwa kufanya ukatili zaidi.

Wasanii kadhaa wa kimataifa wamejitokeza kuunga mkono maandamano hayo

Rihanna aliweka kwenye mtandao wake wa Twitter picha ya bendera ya Nigeria iliyokuwa na damu na kuambatanisha maneno: "Moyo wangu umevunjika kutokana na matukio yanayoendelea Nigeria.

Nikki Minaj alizungumza na waandamanaji moja kwa moja katika Twitter yake, akisema: "Sauti yenu inasikika".

Halafu ikafuata kauli ya Beyoncé

Kupitia shirika lake la misaada la, BeyGood, alisema: "Nimevunjika moyo kuona unyama usiokuwa na maana unafanyika nchini Nigeria ... tunashirikiana na miungano kutoa huduma za dharura za afya, chakula na malazi. "

Kauli hiyo haikupokelewa vyema na waandamanaji.

"Nani alimwambia Beyoncé tuna njaa?" alitoa maoni mjasiriamali wa kidijitali Papi Jay.

Ruka Twitter ujumbe, 5

Who told Beyonce that we are hungry? Sis just lend your voice like Riri and co.

— Papi Jay (@JohnMarsAuto) October 21, 2020

Mwisho wa Twitter ujumbe, 5

Maoni yake yaliungwa mkono na muuzaji wa vipodozi Mercy Ehimare. "kuna mtu anaweza kumwambia mwanamke huyu hatuna njaa??????? Tunahitaji msaada kupigania haki yetu, "alijibu.

Kwa nini watu wanaandamana?

Maandamano yalianza karibu wiki mbili zilizopita kushinikza kuvunjiliwa mbali kwa kitengo maalum cha polisi cha kukabiliana na wizi wa mabavu (Sars).

Kitengo hicho kimetuhumiwa kuwazuilia watu kinyume cha sheria, kuwanyanyasa na kuwa kuwapiga risasi na kilivunjwa na Rais Muhammadu Buhari Oktoba tarehe 11.

Lakini maandamano yameendelea kushuhudiwa katika maeneo kote nchini, miito ya kutaka huduma za usalama kufanyiwa mageuzi pamoja na serikali kwa ujumla.

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kumeshuhudiwa ongezeko la watu wanaounga mkono maandamano ya Nigeria kupitia mtandao wa Twitter, kupitia hashtag tofauti, lakini ile iliyopata umaarufu ni ya #EndSARS.

Maandamano hayo wakati mwingine yamekubwa na vurugu. Siku ya Jumanne shirika la kutetea haki la Amnesty International lilisema makundi ya watu waliojihami yalishambulia watu katika mji mkuu, Abuja.

Kampeni ya #EndSARS imepata umaarufu kwenye mitandao kote ulimwenguni. Picha: REUTERS
Kampeni ya #EndSARS imepata umaarufu kwenye mitandao kote ulimwenguni. Picha: REUTERS

Kwa upande wao pilisi wamewalaumu watu kwa "kujifanya" waandamanaji na kuiba silaha na kuchoma moto ofisi za polisi katika jimbo la kusini la Edo.

Katika hotuba ya video siku ya Jumatatu, Rais Buhari alisema maafisa wa polisi waliojihusisha na visa vya uvunjifu wa sheria watachukuliwa hatua za kisheria na kuongeza kwamba kuvunjwa kwa kitengo cha Sars ni "hatua ya kwanza katika jitahada za serikali za kufanya mageuzi katika idara ya polisi".

 

BBC