Tanzania; kivumbi kati ya Magufuli na Tundu Lisu

Muhtasari

• Foleni ndefu zashuhudiwa huku wananchi wakichagua rais na vyiongozi wengine.

• Matokeo yanatarajiwa katika muda wa wiki moja.

•Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli apiga kura yake mjini Dodoma

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

Shughuli ya upigaji kura inaendelea nchini Tanzania kwenye uchaguzi unaokisiwa kuwa na upinzani mkubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo huku rais Pombe Magufuli akipiga kura yake katika eneo la Dodoma.

Kulikuwa na kizaazaa katika Kisiwa cha Zanzibar baada ya ripoti kudai kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani lakini hali imetulia.

Wapigaji kura wana hadi saa kumi jioni kupiga kura huku matokeo ya uchaguzi yakitarajiwa kutangazwa katika muda wa wiki moja.

 

Rais John Magufuli ambaye chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza Tanzania kwa miongo kadhaa anatafuta mhula wake wa pili na wa mmwiisho.

Hata hivyo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani Tundu Lisu ambaye chama chake cha CHADEMA ndicho kikubwa kwa upande wa upinzani.  

Lisu aliponea jaribio la mauaji miaka mitatu iliyopita, alirejea nchini Tanzania kutoka Ubelgiji mwezi Julai alikokuwa akipokea matibabu kutokana na majeraha ya risasi aliyopata.

Jumla ya wagombeaji 15 wanawania kiti cha urais akiwemo aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe aliyekihama chama cha CCM na sasa anakiongoza chama cha ACTS Wazalendo.