Uchaguzi wa Marekani

Biden asema Trump anatuma ujumbe mbaya kwa kukataa matokeo

Trump amezidi kusema kulikuwa na udanganyifu

Muhtasari
  • Kulikuwa na marudio ya kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika jimbo la Georgia, na bwana Biden alipata ushindi katika jimbo hilo.
  • Alikuwa akiongea katika mkutano wa simu na magavana , wakiwemo wa Democrats na Republicans, kuhusu janga la corona.

 

Picha: GETTY IMAGES
Picha: GETTY IMAGES

 Rais mteule wa Marekani Joe Biden amelaani kitendo cha Donald Trump kukubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais, amesema kuwa 'anatuma ujumbe mbaya sana kuhusu Marekani'.

Bwana Biden amesema, alikuwa na uhakika kuwa bwana Trump alikuwa anajua kuwa hangeshinda na kila kitu kilionekana wazi , kwa kuwa alikuwa hajitumi kabisa katika majukumu yake.

Kulikuwa na marudio ya kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika jimbo la Georgia, na bwana Biden alipata ushindi katika jimbo hilo.

Bwana Trump alifungua kesi  kadhaa za  madai ya wizi wa kura.

Madai yake yote ya kisheria yaligonga mwamba na kushindwa kufanya mabadiliko yoyote.

Bwana Biden amepata ushindi wa kura za umma kwa zaidi ya milioni 5.9 .

Ushindi wake katika kura za wajumbe ambazo zinaweza kuthibitisha nani anakuwa rais aliweza kukadiriwa kupata kura 306 mpaka 232.

Alikuwa akiongea katika mkutano wa simu na magavana , wakiwemo wa Democrats na Republicans, kuhusu janga la corona.

Alihojiwa kuhusu suala la Trump kutokubali ushindi wake, Biden alisema rais anatuma ujumbe wa kutisha... kwa dunia nzima kuhusu jinsi demokrasia inavyofanya kazi, na hilo anapaswa kulikumbuka kwa kuwa amekuwa rais ambaye hawajibiki katika historia ya Marekani."

"Ni suala gumu kufahamu jinsi mtu anavyofikiri ," aliongeza: "Jambo ambalo analifanya linaleta hasira."

 

Matokeo ya uchaguzi wa rais, rais mteule huyo kutoka Democratic anaapishwa kuingia madarakani mwezi Januari.

Alhamisi, Katibu wa jimbo la Georgia, Brad Raffensperger, alisema kuwa kura urudiwaji wa kura haujabadilisha ushindi wa Biden katika jimbo hilo.

Awali, Republicans walishindwa kesi yao baada ya mahakama kukataa kusitisha kutoa cheti cha kukubali uchaguzi, na kinatarajiwa kutolewa Ijumaa.

Marudio ya kuhesabu kura walipata makosa ya kiwango cha juu kwa 0.73% kati ya Biden na Trump na kiwango cha chini kilisalia kuwa chini ya 0.5%.