- Don Junior amekosolewa kwa kupuuza athari za Corona
- Babake na mamake wa kambo Melania ni miongoni mwa walioambukziwa hapo awali
Mwanawe wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump amepatikana na virusi vya corona kulingana na msemaji .
Donald Trump Jr, mwenye umri wa miaka 42 alipatikana na ugobnjwa huo mwanzoni mwa wiki hii na amekuwa akijitenga katika karantini tangu matokeo hayo yalipotolewa .
" Hajakuwa na daalili zozote na anafuata kanuni zote za matibabu kuhusu covid 19’ imesema taarifa iliyotolewa
Don Jr ni mtoto wa pili wa Trump kupatikana na virusi hivyo bada ya Barron Trump mwenye umri wa miaka 14 kupatikana na ugonjwa huo mwezi uliopita lakini sasa amepona .
Don Junior alikuwa nguzo muhimu sana katika kampeini za babake na kumekuwa na uvumi kwamba naye pia angependa kugombea urais siku zijazo .
Mpenzi wake Don Jr ,Kimberly Guilfoyle, aliyekuwa akitangaza katika kituo cha Fox alipatikana na virusi hivyo mwezi Julai na pia akapona .Hakupata ugonjwa huo wakati huo .
Mapema siku ya ijumaa msaidizi maalum wa rais Andrew Giuliani, alitangaza pia kwamba amepatikana na virusi vya corona .
Mr Giuliani, ni mtoto wa wakili wa rais Trump Rudy Giuliani, alisema katika twitter kwamba alikuwa akishuhudia ishara chache za kuugua baada ya kupokea matokeo yake siku ya ijumaa asubuhi .
Mapema mwezi huu mkuu wa wafanyikazi katika White House Mark Meadows alikuwa miongoni mwa maafisa wakuu waliopatikana na virusi vya Corona . Rais Trump mwenyewe alilazwa hospitalini kwa siku tatu mwanzoni mwa mwezi oktoba baada ya kupatikana na virusi hivo .Mkewe Melania Trump pia aliambukizwa na akapona