Biden asema marekani imerejea wakati wa uzinduzi wa timu yake

Muhtasari

Rais Donald Trump amekubali kuanza kwa mchakato wa kukabidhi madaraka.

 

Rais mteule wa Marekani Joe Biden
Rais mteule wa Marekani Joe Biden

Uchagizi wa Marekani 2020: 'Marekani imerejea tena', amesema Biden wakati anazindua timu yake Rais mteule Joe Biden ajaza nafasi sita muhimu akisubiri kuapishwa na kuchukua rasmi madaraka.

"Marekani imerejea katika hali yake", amesema, na "iko tayari kuongoza dunia, bado haijakata tamaa".

Ikiwa watathibitishwa, Avril Haines atakuwa mkurugenzi wa kwanza mwanamke katika shirika la upelelezi wa taifa na Alejandro Mayorkas kuwa waziri wa kwanza wa Mambo ya ndani Mlatino.

 

Donald Trump amekubali kuanza kwa mchakato wa kukabidhi madaraka na Bwana Biden sasa atapewa taarifa kutoka shirika la Upelelezi wa Taifa.

Hata hivyo, rais Trump bado amekataa kukubali kuwa alishindwa na kurejelea madai ya uwepo wa wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba 3.

Pia ataanza kupata taarifa za kila siku kama ilivyo kwa rais - taarifa kuhusu vitisho vya kimataifa na maendeleo - Bwana Biden sasa anaweza kuwasiliana na maafisa wa ngazi ya juu serikalini na kufikia mamilioni ya madola wakati anajitayarisha kuchukua rasmi madaraka Januari 20.

Jumanne, Gavana Tom Wolf alisema amemuidhinisha Bwana Biden kama mshindi wa jimbo la Pennsylvania huku akiidhinishwa kupata ushindi wa jimbo la Michigan vilevile siku ya Jumatatu.

Biden alisema nini?

Akizungumza Wilmington, Delaware, rais mteule aligusia haja ya kujenga upya ushirikiano, kukabiliana na virusi vya corona pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Viongozi wa dunia, Biden alisema, "wanafuatilia "kuona Marekani ikichukua tena jukumu lake la kihistoria kama kiongozi wa dunia eneo la Pacific, pamoja na Atlantic, na kote duniani".

 

Akizungumza kupitia shirika la habari la NBC News, alisema: "Rais huyu, Rais Trump, amebadilisha muelekeo. Na kuwa Marekani kwanza, Marekani peke yake. Tumejipata katika hali ambapo washirika wetu wanasononeka."

Bwana Biden pia aliwaambia wanahabari kuwa amezungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kuhusu mpaka wa Ireland pamoja na viongozi wengine wa dunia.

Bwana Biden ambaye ana uhusiano wa karibu na Ireland, alisema anapinga uwepo wa ulinzi katika mpaka wa eneo hilo na kusema kuwa unastahili kuwa wazi: "Wazo la kuanza kufunga tena mpaka wa kaskazini na kusini, sio sawa."

Biden alisema, ana mpango wa kukutana na jopo kazi la kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona katika Ikulu ya Marekani kuhusu kuanza kutolewa kwa chanjo na upatikanaji wake.

Biden aliyekuwa makamu rais wa Barack Obama amesema wakati wake uongozini hautakuwa "muhula tatu wa Obama" kwasababu "tuko katika dunia tofauti kabisa na tuliokabiliana nayo wakati wa utawala wa Obama na Biden".

Walioteuliwa ni kina nani?

Bwana Biden alimchagua jake Sullivan , Linda Thomas na Anthony Blinken kuchukua majukumu muhimu. GETTY IMAGES
Bwana Biden alimchagua jake Sullivan , Linda Thomas na Anthony Blinken kuchukua majukumu muhimu. GETTY IMAGES

Biden alifanya uteuzi wa majina sita katika nyadhifa muhimu:

•Antony Blinken, Waziri wa mambo ya Nje. Bwana Blinken alisema karibuni Marekani "kwa unyenyekevu na kujiamini" itarejesha tena uhusiano nan chi zingine

•John Kerry, mjumbe wa mabadiliko ya tabia nchi. Alikuwa miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele katika makubaliano ya hali ya hewa ya Paris, ambayo rais Trump alijiondoa. Bwana Kerry dunia inastahili "kushikamana kumaliza mgogoro wa hali ya hewa"

•Avril Haines, Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi. Bwana Biden alisema: "Nimemchagua mtaalamu... mwanaharakati wa kusema ukweli".

•Alejandro Mayorkas, Waziri wa Mambo ya Ndani. Bwana Mayorkas wizara hiyo ina "maono bora, ya kutusaidia kuwa salama na kuendeleza historia ya fahari yetu kama nchi yenye makaribisho mazuri"

•Jake Sullivan, Mshauri wa Masuala ya Usalama Ikulu. Bwana Sullivan alimsifu mkuu wake, akisema amemfunza mengi kuhusu sera lakini pia, "cha muhimua zaidi ni kuhusu ubinadamu"

•Linda Thomas-Greenfield, Balozi wa marekani kwa Umoja wa Mataifa. Alisema alicholeta ni pamoja na diplomasia ya uhakika.

BBC