Mzozo wa Tigray

Komeni kuingilia masuala ya ndani ya Ethiopia,waziri Mkuu Abiy aimabia Jamii ya kimataifa

Acheni tushughulikie mzozo huu-Aby

Muhtasari

 

  •  Abiy na serikali yake wamekataa kuzungumza na wanachama 
  • Nchi nyingi zinahofia mzozo huo utaenea hadi katika mataifa jirani 

 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Aby Ahmed

 Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed  ameitaka jamii ya kimataifa kukoma kuingilia  oparesheni ya  kijeshi inayoendelea katika jimbo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo .

Abiy  siku ya jumatano amesema  jamii ya kimataifa inafaa kuheshimu mmsimamo wa serikali kuu na kusimama nayo hadi itakapoitisha msaada  jamii ya kimataifa .

 Kupitia taarifa amesema  ingawaje Ethiopia inaheshimu uchu uliopo wa jamii ya kimataifa kuleta  Amani nchini humo kupitia njia za upatinisho ,kinachofanyika sasa ni suala la ndani na Ethiopia ikiwa nchi huru inastahili kupewa fursa ya kushughulikia changamoto hizo kivyake .

 Mataifa mengine pamoja na mashirika ya kimataifa yamekuwa yakiitisha kuwepo mazungumzo kati ya serikali ya Abiy na wanachama wa TPLF ambao wanakabiliana katika jimbo la Tigray .

 Siku ya jumane katibu wa masuala ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab akizungumza na rais Uhuru Kenyatta ameelezea hofu ya mzozo wa Tigray kuleta msukosuko katika kanda nzima ya upembe wa Afrika .

Raab  amesema kuna haja ya dharura ya kutafuta suluhisho la kisiasa kwa mzozo huo