Trump afurushwa kutoka Twitter milele

Muhtasari

• Rais wDonald Trump ameondolewa kabisa kutoka mtandao wa Twitter "kwa sababu ya hatari ya kuzidisha vurugu".

• Trump alikuwa amefungiwa nje ya akaunti yake kwa saa 12 siku ya Jumatano baada ya kuwaita watu waliovamia bunge la Marekani, Capital Hill "wazalendo".

Rais wa Amerika Donald Trump ameondolewa kabisa kutoka mtandao wa Twitter "kwa sababu ya hatari ya kuzidisha vurugu", kampuni hiyo inasema.

Twitter ilisema uamuzi huo ulifanywa "baada ya ukaguzi wa karibu wa jumbe zake za hivi karibuni kutoka kwa akaunti ya @realDonaldTrump".

Hatua hii inajiri wakati kuna oparesheni kali ya kusafisha majukwaa ya mtandaoni yanayotumiwa na Bwana Trump na wafuasi wake.

 

Kwanini Trump alipigwa marufuku?

Bwana Trump alifungiwa nje ya akaunti yake kwa saa 12 siku ya Jumatano baada ya kuwaita watu ambao walivamia bunge la Marekani, Capital Hill "wazalendo".

Mamia ya wafuasi wake waliingia katika jengo hilo wakati Bunge la Amerika likithibitisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa rais. Vurugu zilizofuata zilisababisha vifo vya raia wanne na afisa wa polisi.

Twitter ilionya basi kwamba itampiga marufuku Bw Trump "kabisa" ikiwa atakiuka sheria za jukwaa tena.

Baada ya kuruhusiwa kurudi kwenye Twitter, Bwana Trump alichapisha jumbe mbili Ijumaa ambazo kampuni hiyo ilitaja kama msumari wa mwisho kwenye jeneza.

Katika moja ya jumbe hizo, aliandika: "Wazalendo wazuri wa Amerika 75,000 ambao walinipigia kura, AMERICA KWANZA, na KUFANYA AMERICA KUBWA TENA, tutakuwa na SAUTI KUBWA kwa muda mrefu baadaye.

 Twitter ilisema kwamba kulingana na ujumbe huu “ni ishara zaidi kwamba Rais Trump hana mpango wa kuwezesha" mpito mzuri wa mamlaka".

 

Katika tweet nyingine rais alisema: "Kwa wale wote ambao wameuliza, sitakwenda kwenye hafla ya kuapishwa Januari 20."

Twitter ilisema ujumbe huu "ulikuwa ukipokelewa na wafuasi wake kadhaa kama uthibitisho zaidi kwamba uchaguzi haukuwa halali".

Twitter ilisema tweets hizi mbili "zilikiuka Sera ya Kutukuza Vurugu".