Joe Biden aapishwa kuwa rais wa marekani

Muhtasari
  • Joe Biden ameapishwa kuwa rais wa 46 wa marekani
  • Aliyekuwa rais wa 45 Donald Trump hajahudhuria hafla hiyo

Joe Biden amekula kiapo na kuwa rais wa 46 wa taifa la Marekani. Biden amekula kiapo mbele ya jaji wa Mahakama Kuu John Roberts.

Baada ya kula kiapo Biden amelihutubia taifa kwa mara ya kwanza akiwa Rais wa Marekani akisema ''hii ni siku ya kidemokrasia''.Siku ya kihistoria na matumaini.

''Marekani imejaribiwa na kunyanyuka tena dhidi ya changamoto. Leo tunasheherekea ushindi si wa mgombea isipokuwa ushindi wa demokrasia

 

Ninawashukuru watangulizi wangu wa vyama vyote walio hapa hii leo.'' alisema Rais mpya. Marais wa zamani Clinton.

Bush na Obama wamehudhuria sherehe hiyo.

Biden amesema alizungumza kwa njia ya simu na Rais Jimmy Carter- ambaye sasa ana miaka 96, na kumpongeza kwa utumishi wake.

Mtangulizi wake, Donald Trump hajahudhuria tukio hilo muhimu.