Mzozo wa Tigray Ethiopia: Ssi ni serikali na tunajua unachofanya

Muhtasari

Mwandishi wa BBC asimulia aliyopitia baada ya kamatwa

Mwandishi wa BBC Girmay Gebru, ambaye alikuwa miongoni mwa wanahabari kadhaa waliozuiliwa Mekelle, mji mkuu waJimbo la Tigray linalokumbwa na mzozo nchini Ethiopia, aelezea kilichomkuta:

Nilikamtwa mkesha wa siku yangu ya kuzaliwa.

Nilidhani maaskari waliokuwa wamejihami kwa silaha, walikua wakimtafuta mtu walipozingira duka la kahawa ambapo nilikuwa nikikutana mara na marafiki siku ya Jumatatu.

 

MMoja wa maafisa hao alikuja na kuwaambia watu wawe watulivu nasi tukaendelea na gumzo letu. Lakini dakika chache baadae, tulifuatwa na maajenti wa kintelijensia waliokuwa wamevalia nguo za nyumbani.

"Nyini ni kina nani?" moja wao aliuliza kwa sauti.

"Tuambieni majina yenu!"

"Mini ni Girmay Gebru," Nilisema.

"Ndio wewe, wewe ndio mtu tunayemtakat." Na hapo tukachukuliwa pamoja na marafiki zangu watano.

Kisha mbele ya watu waliokuwa wakifuatilia tukio hilo, mmoja wa maafisa hao wa intelijensia alinizabwa kofi usoni hata baada ya mimi kuwasilisha kitambulisho changu cha kitaifa na kitambulisho cha kazi cha BBC

Askari mwengine aliingialia kati na kumuomba asinipige na baada ya hapo niliingizwa kwenye gari na kuondoka.

Mambo yalifanyika haraka kiasi cha kuwa nilisahau kuulizia kwanini nimekamatwa.

Huu sio uchunguzi bali ni onyo tu.

Tulirudishiwa simu zetu ambazo zilikuwa zimechukuliwa na maafisa wa jeshi na kuambiwa tupige simu moja

Mke wangu aliingiwa na wasiwasi nilipomueleza kilichotokea lakini nikamwambia asiwe na wasiwasi

1px transparent lineHatukusumbuliwa katika kambi hiyo, lakini sote tulilala sakafuni katika chumba kimoja na kupewa ndoo za plastiki kutumia kama choo.

Sote tulikuwa na wasi wasi ni nini kitakachofuata. Sikupata lepe la usingizi.

Asubuhi ilipofika, maafisa wa intelijensia waliniambia wanataka kupekua nyumba yangu na kwamba watachukua kombuyuta na simu yangu ili kupakua data zote kutoka kwa vifaa hivyo. Lakini baadae nilifahamu kuwa hawakupekua nyumba yangu kama walivyosema.