Kanisa katoliki haliwezi kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja

Muhtasari
  • Kanisa katoliki halina uwezo wa kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja, afisa wa mafundisho mjini Vatican amesema
  • Haiwezekani kwa Mungu kubariki dhambi, ofisi inayokutana kutoa mafundisho imesema siku ya Jumatatu

Kanisa katoliki halina uwezo wa kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja, afisa wa mafundisho mjini Vatican amesema.

Haiwezekani kwa Mungu kubariki dhambi, ofisi inayokutana kutoa mafundisho imesema siku ya Jumatatu.

Hata hivyo ofisi ya mkutano huo ilitambua kwamba kuna mambo mazuri katika mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja.

 

Mwezi Oktoba, Papa Francis alisema katika makala moja kwamba alifikiria kwamba ndoa za wapenzi wa jinsia moja zinapaswa kuhalalishwa.

Papa Francis anaonesha kuunga mkono vyama vya wapenzi wa jinsia moja, Katika Kanisa Katoliki, baraka hutolewa na kuhani au mhudumu mwingine kwa jina la Kanisa.

Mwaka 2013 papa Francis alivunja mafundisho akisema kwamba '' Mimi ni nani kuwahukumu wapenzi wa jinsia''?

Siku ya Jumatatu papa Francis aliidhinisha jibu la mkutano wa mafundisho, akisema kwamba sio njia ya kuwabagua, badala yake ni ukweli.

"Baadhi ya parokia katika miezi ya hivi karibuni, ikiwemo Ujerumani na Marekani zimeanza kuwabariki wapenzi wa jinsia moja kama njia ya kuwakaribisha wakatoliki wapenzi wa jinsia moja katika kanisa hilo,"Kitengo cha habari ya reuters .

Jibu hilo la CDF lilitokana na jibu kutoka kwa swali lililoulizwa.

Je kanisa hilo lina uwezo kutoa baraka kwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja? Lilijibu hapana.

 

Mkutano wa mafundisho hayo ulisema kwamba ndoa kati ya wanaume na wanawake ni sakramenti na hivyo basi baraka haziwezi kupewa wapenzi wa jinsia.

Kwa sababu hiyo, sio makosa kutoa baraka kuhusu mahusiano, au ushirikiano m hata yalio thabiti ambayo uhusisha vitendo vinavyohusisha tendo la ndoa nje ya ndoa.