SIASA ZA TANZANIA

Tanzania: Kiongozi wa upinzani ataka Rais Samia kueleza ukweli kuhusu jaribio la mauaji

Lissu alifanyiwa upusuaji kwa mara ya 25 baada ya kupigwa marisasi 16 yaliyompata kwenye miguu, mikono na kwenye tumbo mwakani 2017

Muhtasari

•Baada ya hayo kutukia, Lissu alienda mafichoni nchini Ubelgiji na kurudi Tanzania miaka tatu baadae ili kuwania kiti cha Urais. 

•Lissu amemtaka Rais Samia kueleza tukio hilo kuona kuwa kwa wakati ule alikuwa naibu rais kwenye serikali ya Rais Magufuli.

Tundu Lissu Hospitalini
Tundu Lissu Hospitalini
Image: Hisani

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Antiphas Lissu amemuagiza Rais Samia Suluhu kueleza taifa ukweli kuhusu nani aliyekuwa ameamuru kuuliwa kwake na kwa nini.

Alipokuwa anatangaza mafanikio katika upasuaji wake wa mara ya 25 siku ya Jumanne, kufuatia jaribio la mauaji lililofanyika miaka minne iliyopita, Lissu alisema kuwa kimya cha Rais Samia kinahofisha.

"Leo nimefanyiwa upasuaji wa mara ya 25 kufuatia jaribio la mauji lililofanyika tarehe Septemba 7, 2017. Huku Magufuli akiwa ameenda, ni wakati rais mpya Samia aniambie na aambie taifa ni nani aliyekuwa nyuma ya kupigwa marisasi kwangu na kwa nini? nani alipeana amri? Kimya chake hakiwezi vumiliwa tena!" Lissu aliandika kwenye mtandao wa Twitter.

Katika tukio hilo, Lissu alivamiwa na kikundi cha wauaji wawili waliopiga gari lake marisasi alipokuwa anawasiri nyumbani kwake akitokea kwenye kikao cha bunge mjini Dodoma.

Lissu alipokea marisasi 16 yaliyompata kwenye miguu, mikono na kwenye tumbo. Hata hivyo, alinusurika na kupelekwa katika hospitali ya Aghakan nchini Kenya ambako alipokea matibabu.

Mwanasiasa huyo ambaye aliwania kiti cha urais nchini Tanzania mwaka uliopita bila mafanikio alilaumu serikali kwa jaribio hilo huku akisema kuwa siku hiyo walinzi walikuwa wameondolewa kwenye boma lake ili kufanikisha mauaji hayo. Kwa wakati huo Lissu alikuwa kiranja wa wapinzani katika bunge la kitaifa.

Baada ya hayo kutukia, Lissu alienda mafichoni nchini Ubelgiji na kurudi Tanzania miaka tatu baadae ili kuwania kiti cha Urais. Hata hivyo, alibwagwa chini na Hayati Rais Magufuli aliyega mapema mwakani.

Lissu amemtaka Rais Samia kueleza tukio hilo kuona kuwa kwa wakati ule alikuwa naibu rais kwenye serikali ya Rais Magufuli.