UONGOZI WA ISRAELI

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ang'atuliwa mamlakani

Netanyahu amepoteza utawala wake wa miaka 12 madarakani nchini Israeli baada ya bunge la taifa hilo kupiga kura ya kuidhinisha serikali mpya ya muungano.

Muhtasari

•Bwana Bennett atakuwa waziri mkuu hadi mwezi Septemba 2023 ikiwa ni maafikiano ya ugavi wa mamlaka.

•Bwana Netanyahu amehudumu kwa rekodi ya mihula mitano , mara ya kwanza kuanzia mwaka 1996 hadi 1999, na baadaye kuendelea kutoka mwaka 2009 hadi 2021.

Benjamin Netanyahu
Benjamin Netanyahu
Image: Hisani

Hatimaye Benjamin Netanyahu amepoteza utawala wake wa miaka 12 madarakani nchini Israeli baada ya bunge la taifa hilo kupiga kura ya kuidhinisha serikali mpya ya muungano.

Kiongozi wa mrengo wa kulia, Naftali Bennet ameapishwa kuwa waziri mkuu mpya akiongoza “serikali ya mageuzi”

Ataongoza muungano wa vyama ulioidhinishwa kupitia uongozi mwembamba wa walio wengi wa 60-59.

Bwana Bennett atakuwa waziri mkuu hadi mwezi Septemba 2023 ikiwa ni maafikiano ya ugavi wa mamlaka.

Baadaye atamkabidhi Yair Lapid - kiongozi wa chama cha mrengo wa kati cha Yesh Atid, kuongoza kwa miaka mingine miwili.

Bwana Netanyahu - kiongozi aliyeongoza kwa muda mrefu ambaye ametawala siasa za taifa hilo kwa miaka kadhaa atasalia kuwa kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud na kuwa kiongozi wa upinzani.

Netanyahu Kushoto na Bennet Kulia
Netanyahu Kushoto na Bennet Kulia
Image: Hisani

Wakati wa mjadala katika bunge la Knesset , bwana Netanyahu ambaye hakukubali kushindwa aliahidi: ''Tutarudi''.

Baada ya kura hiyo kupigwa , Bwana Netanyahu alisimama na kumkaribia bwana Bennett kabla ya kumuamkua kwa mkono.

Rais wa Marekani Joe Biden tayari ametuma risala za pongezi kwa bwana Bennett , akisema kwamba yuko tayari kufanya kazi naye.

Kwanini hilo limefanyika?

Allitisha uchaguzi 2019 lakini akashindwa kupata uungwaji mkono wa kutosha ili kuunda serikali mpya ya muungano 

Kulifanyika chaguzi nyengine mbili baadaye ambazo zilikamilika bila kupata mshindi wa moja kwa moja.

Uchaguzi wa tatu ulipelekea kuundwa kwa serikali ya muungano ambapo bwana Netanyahu alikubali kugawa mamlaka na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Benny Gantz.

Lakini mpango huo ulishindwa kufua dafu mwezi Disemba na kusababisha uchaguzi wa nne.

Ijapokuwa chama cha Likud kilijitokeza kama chama kikubwa katika bunge la Knesset lenye viti 120, bwana Netanyahu kwa mara nyengine alishindwa kuunda serikali ya muungano na jukumu hilo likapewa bwana Lipid, ambaye chama chake cha mrengo wa kati cha Yesh Atid kilikuwa cha pili kwa ukubwa.

Upinzani uliokuwa ukipinga utawala wa Netanyahu madarakani uliongezeka , sio tu miongoni mwa vyama vya mrengo wa kushoto na ule wa kati bali pia miongoni mwa walio katika mrengo wa kulia ambavyo vina mawazo sawa na chama cha mrengo wa kulia cha Likud ikiwemo Yamina.

Ijapokuwa chama cha Yamina kilikuwa cha tano katika uchaguzi huo kikiwa na viti saba pekee, uungwaji mkono wake ulikuwa muhimu iwapo serikali yoyote ya muungano ingetaka kuwa na wingi wa wabunge bungeni.

Wanaisraeli
Wanaisraeli
Image: Hisani

Je serikali mpya itakuwaje?

Kwa muonekano serikali ya bwana Bennett itakuwa tofauti na zile za watangulizi wake katika historia ya Israel ya miaka 73.

Muungano huo unashirikisha vyama ambavyo vina tofauti kubwa ya kimawazo , na pengine kitu muhimu ni kuwepo kwa chama huru cha Kiarabu kuwa ndani ya muungano huo , Raam.

Muungano huo pia utavunja rekodi ya kuwa na mwaziri wanawake wengi zaidi .

Kushirikishwa kwa Raam na vyama vya mrengo wa kushoto ambavyo sio vya Waarabu wala Waisraeli kama kile chenye sera za Israel zinazounga mkono Palestina -Yamina na chama chengine cha mrengo wa kulia , New hope , ni vyama vinavyoungwa mkono walowezi wa Kiyahudi katika maeneo yanayokaliwa ya ukanda wa magharibi kwa mfano.

Pia huenda kukawa na ugumu kuhusu sera za kutangamana huku baadhi ya vyama vikipigania haki za wapenzi wa jinsia moja kama ndoa za wapenzi wa jinsia moja , Raam ambacho ni chama cha Kiislamu kinapinga hilo.