•Wanaume ishirini na moja wameuawa katika jimbo lenye uhuru wa Somalia la Puntland baada ya kupatikana na hatia ya kuwa wanachama wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab.
•Walihukumiwa na mahakama ya kijeshi huko Galkayo na kupigwa risasi na kikosi maalum kilichojihami kwa bunduki .
Wanaume ishirini na moja wameuawa katika jimbo lenye uhuru wa Somalia la Puntland baada ya kupatikana na hatia ya kuwa wanachama wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab.
Walihukumiwa na mahakama ya kijeshi huko Galkayo na kupigwa risasi na kikosi maalum kilichojihami kwa bunduki .
Redio ya serikali ilisema kuwa 18 kati yao walikuwa wametekeleza mauaji na ulipuaji wa mabomu kwa zaidi ya muongo mmoja.
Hukumu kama hizo za kifo zilikuwa zimetolewa na mahakama katika maeneo mengine ya Somalia hapo awali.
Lakini hii inaripotiwa kuwa idadi kubwa zaidi ya mauaji ya wafuasi wa al-Shabab kuwahi kutokea Puntland.
Mamlaka huko Puntland zilikuwa zimeapa kuwafikisha mahakamani wafuasi wa al-Shabab au watu watakaopatikana wakisaidia kundi hilo katika mashambulio yake.
(Maongezi: Samuel Maina)