Jimbo la Nigeria lafunga shule kutokana na utekeji nyara

Muhtasari
  • Vikosi vya usalama kwa sasa vinawasaka watekaji nyara ili kuwaokoa wahanga
  • Awali, majimbo kadhaa kaskazini mwa Nigeria yalifunga shule zake lakini hilo halikutatua mzozo wa utekeji nyara
Image: BBC

Maafisa katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kaduna wameamrisha kufungwa mara moja kwa shule katika maeneo yanayokabiliwa na hatari ya mashambulio.

Hii inakuja simu moja baada ya watu wenye silaha kuwateka nyara wanafunzi 150 kutoka shule ya sekondari katika jimbo hilo. Katika tukio jingine tofauti mama mmoja na mtoto mchanga walichukuliwa kutoka hospitali.

Vikosi vya usalama kwa sasa vinawasaka watekaji nyara ili kuwaokoa wahanga.

Kamishna wa jimbo laKaduna wa elimu, Shehu Usman Muhammad, ameiambia BBC kwamba shule zote zilizopo zaidi yaumbali wa dakika 30 kwa gari kutoka kwenye kituo cha usalama zimeamrishwa kufungwa hadi mipango mingineya usalamaitakapofanywa.

Haiko wazi ni hatua gani mpya zitakazochukuliwa huku serikali ikionekana kulemewa na hali mbaya ya usalama inayoendelea kuenea nchini humo.

Awali, majimbo kadhaa kaskazini mwa Nigeria yalifunga shule zake lakini hilo halikutatua mzozo wa utekeji nyara.