Maelfu wapanga foleni kumuaga mhubiri TB Joshua

Muhtasari
  • Mwili wake umekuwa katika kanisa Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) huko Lagos ambapo atazikwa Ijumaa
  • Siku ya jumanne Viongozi na watu mbali mbali maarufu walikuwa katika makao makuu ya kanisa la TB Joshua ili kutoa heshima na rambi rambi zao 
Image: BBC

Waombolezaji wamejitokeza kwa wingi kuona mwili wa mhubiri mwenye ushawishi mkubwa wa Nigeria TB Joshua, aliyekufa mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 57.

Mwili wake umekuwa katika kanisa Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) huko Lagos ambapo atazikwa Ijumaa.

Ibada za mazishi zilianza na misa ya kuwasha mishumaa siku ya Jumatatu na kulikuwa misa nyingine siku ya jumanneya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho .

TB Joshua alikuwa mmoja wa wainjilisti maarufu nchini Nigeria .Makumi ya maelfu ya watu Walihudhuria misa za kila wiki huko Lagos.

Umaarufu mwishoni mwa miaka ya 1990 uliwiana na mlipuko wa vipindi vya "miujiza" vilivyopeperuhwa kwenye runinga ya kitaifa na wachungaji mbali mbali

Kanisa lake lilidai kuponya kila aina ya magonjwa pamoja na VVU / Ukimwi na kuvutia watu kutoka kote ulimwenguni.

Image: BBC

Siku ya jumanne Viongozi na watu mbali mbali maarufu walikuwa katika makao makuu ya kanisa la TB Joshua ili kutoa heshima na rambi rambi zao .

Mke wake Evelyne na watoto wake watatu Sarah, Promise and Heart walipata fursa ya kumzungumzia maisha ya TB Joshua.

Kulingana na mke wake Evelyn Joshua, alishuhudiaTB Joshua akikua ‘’kutoka kuwa na kusanyiko la waumini 8 wa kanisa hadi kuwa na kanisa lililojaa umati wa watu na kuwa na wafuasi kote duniani "

‘’Alinifunza kuwa mwanamke niliye leo. Kwa dhahabu kuwa dhahabu lazima ipitie moto. Ninataka tu kukushukuru kwa kuwa baba mwema wa watoto wetu.", alisema mjane Everlyne.

Watoto wake TB Joshua , Sarah, Promise na Heart walimsifu baba yao mpendwa kwa kuwa mtu aliyejitolea kumtumikia Mungu " kwa heshima bila uwoga."

"Aina ya upendo uliotuonesha hatukuwahi kuuona maishani mwetu. Kama kuna mtu yeyote aliyeishi maisha ya kushangaza ni wewe. Baba yangu alikuwa na utu ambao kwa namna ambayo sikuwahi kuelewa kamwe ," alisema binti yake Sarah.

Mchakato wa mazishi ya kumuaga na kumkumbuka TB Joshua ulianza Jumatatu .