Maandamano yashika kasi Afrika Kusini kufuatia kukamatwa kwa Zuma

Watu takribani 800 walihusika kwenye tukio ambalo afisa wa polisi alipigwa risasi huko Alexandra

Picha zimeonesha majengo na magari yakiwaka moto.
Picha zimeonesha majengo na magari yakiwaka moto.

Makumi ya watu wamekamatwa nchini Afrika Kusini huku ghasia zikienea kufuatia kufungwa jela kwa rais wa zamani Jacob Zuma.

Waandamanaji wanaomuunga mkono Zuma kwanza waliingia mitaani baada ya kiongozi huyo wa zamani 79 kujisalimisha kwa mamlaka Jumatano ili kuanza kifungo cha miezi 15.

Lakini polisi sasa wanasema wahalifu wanachukua fursa ya machafuko, ambayo yalisambaa kutoka mkoa wake wa KwaZulu-Natal hadi Johannesburg, huko Gauteng.

Picha zimeonesha majengo na magari yakiwaka moto.
Picha zimeonesha majengo na magari yakiwaka moto.

Idara ya intelijensia, imesema watu 300 waliandamana barabara kuu mjini Johannesburg nchini humo.

Watu takribani 800 walihusika kwenye tukio ambalo afisa wa polisi alipigwa risasi huko Alexandra. Maafisa wawili walijeruhiwa.

Polisi pia walijibu ripoti za unyang'anyi jijini Johannesburg na KwaZulu Natal. Zaidi ya watu 60 wamekamatwa mpaka sasa.

Haijulikani kama wanahusika na maandamano yanayomuunga mkono Zuma, huku msemaji wa polisi wa KwaZulu-Natal Jay Naicker akiliambia shirika la Reuters kuwa wameshuhudia ''wahalifu wakijaribu kutumia hali ya vurugu za maandamano kujitajirisha''.

Image: EPA

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumamosi aliwataka raia kuwa na utulivu, lakini waandamanaji wakiwa na fimbo na marungu na matawi waliandamana Jumapili jijini Johannesburg.

Zuma amehukumiwa kifungo kwa makosa ya kudharau mahakama , baada ya kushindwa kuhudhuria kesi yake kuhusu rushwa.

Zuma anakana shutuma dhidi yake na hakutoa ushirikiano wakati mchakato wa kisheria ulipokuwa ukiendelea