YAWEZEKANA KENYA?

(+Video)"Tunataka kazi sio mchele!" Vijana warejesha msaada wa mchele waliopatiwa na mwanasiasa

Kupatiana pesa, chakula, nguo au bidhaa zingine ni njia moja inayotumiwa sana na wanasiasa kuwahadaa wapiga kura haswa barani Afrika.

Muhtasari

•Video moja inayoonyesha kikundi cha vijana nchini Ghana kikirejesha gunia za mchele walizokuwa wanapatiwa  na mwanasiasa mmoja imeibua mdahalo mkubwa miongoni mwa Wakenya mitandaoni.

•Vijana hao walisikikia walisikika wakisema  kuwa wanataka kazi sio mchele.

Image: HISANI

Kupatiana pesa, chakula, nguo au bidhaa zingine ni njia moja inayotumiwa sana na wanasiasa kuwahadaa wapiga kura haswa barani Afrika.

Huku kampeni za uchaguzi mkuu wa 2022 zikitarajiwa kuanza karibuni nchini Kenya ni dhahiri kuwa wanasiasa wengi wanaandaa mifuko yao ili kushawishi wananchi kuwapigia kura.

Hilo ni jambo ambalo vijana nchini Ghana wameonekana kupigana nalo huku wakidai kuwa wanataka kazi sio msaada.

Video moja inayoonyesha kikundi cha vijana nchini Ghana kikirejesha gunia za mchele walizokuwa wanapatiwa  na mwanasiasa mmoja imeibua mdahalo mkubwa miongoni mwa Wakenya mitandaoni.

Kwenye video hiyo, vijana wenye ghadhabu walionekana wakitupa gunia hizo  kuzirejesha ndani ya gari aina ya 'pick up' lililokuwa limezibeba.

Vijana hao walisikikia walisikika wakisema  kuwa wanataka kazi sio mchele.

"Tunataka kazi sio mchele... kazi sio mchele!" Vijana hao walisema.

Je, Kenya tumefikia hapo pa kukataa misaada na kudai yale yanayotufaidi? 

Hizi hapa hisia za baadhi ya Wakenya;-