Zuma aruhusiwa kuhudhuria mazishi ya kaka yake

Bw Zuma havai sare ya wafungwa wakati wa “likizo ya msamaha

Muhtasari

•Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa ruhusa ya kuhudhuria mazaishi ya kaka yake mdogo, Michael, ambaye anapangwa kuzikwa Alhamisi mchana.

•Kufungwa kwake kuliibua ghasia katika jimbo la kwao la KwaZulu-Natal na Gauteng – ambako zaidi ya watu 200 waliuawa na mamia ya maduka na biashara kuporwa na kuharibiwa.

Jacob Zuma
Jacob Zuma
Image: REUTERS

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa ruhusa ya kuhudhuria mazaishi ya kaka yake mdogo, Michael, ambaye anapangwa kuzikwa Alhamisi mchana.

‘’Maombi ya Bw Zuma ya msamaha kama mfungwa wa muda mfupi, mwenye kiwango cha chini cha hatari yalishugulikiwa na kuidhinishwa ," alisema msemaji wa idara ya huduma za magereza , Singabakho Nxumalo, alisema Alhamisi.

Bw Zuma havai sare ya wafungwa wakati wa “likizo ya msamaha ”, huku Bw Nxumalo akisema wafungwa hawahitaji kuwa wamevaa sare za jwafungwa wanapokuwa nje ya gereza .

Rais huyo wa zamani kwa sasa anahudumia kifungo cha miezi 15 jela kwa kosa la kutoheshimu agizo la mahakama.

Kufungwa kwake kuliibua ghasia katika jimbo la kwao la KwaZulu-Natal na Gauteng – ambako zaidi ya watu 200 waliuawa na mamia ya maduka na biashara kuporwa na kuharibiwa.