Afghanistan:Mlipuko watokea uwanja wa ndege wa Kabul

Muhtasari

Kumetokea mlipuko nje ya uwanja wa ndege wa mjini Kabul, Pentagon imethibitisha.

Kumetokea mlipuko nje ya uwanja wa ndege wa mjini Kabul, Pentagon imethibitisha.

Taarifa zaidi kuhusu mlipuko huo katika uwanja wa ndege bado hazijafahamika. Kumekuwa na ripoti za kusikika kwa milio ya risasi.

Mlipuko umetokea katika lango la kuingilia la abbey ambako vikosi vya Uingereza vimekuwa katika eneo hilo siku za karibuni.

Ni moja kati ya milango mitatu iliyokuwa imefungwa baada ya kuwepo tahadhari ya tishio la kigaidi.

Afisa wa Marekani ameliambia Shirika la habari la Reuters kuwa mlipuko huo ulisababishwa na mtu aliyejitoa muhanga.

Kulingana na maafisa wa wa Taliban angalu watu 13 wameaga dunia kutokana na mlipuko huo.