Onyo la shambulio la ugaidi limetolewa katika uwanja wa ndege wa Kabul

Nchi zinanahangaika kuondoa raia wao kabla yam udo wa mwisho uliowekwa wa Agosti 31.

Muhtasari

• Zaidi ya watu 82,000 wameondolewa Kabul, ambako wanamgambo wa Taliban wamechukua udhibiti siku 10 zilizopita.

• Nchi zinanahangaika kuondoa raia wao kabla yam udo wa mwisho uliowekwa wa Agosti 31.

Image: Reuters

Mataifa kadhaa yanasema kuna tisho la hali ya juu la kutokea kwa shambulio la kigaidi katika uwanja wa ndege wa Kabul na kuonya raia wao wasisafiri kuelekea huko.

Australia, Marekani na Uingereza zimetoa tahadhari kwa raia wao. Wale waliokuwa nje ya uwanja wa ndege wameshauriwa kuondoka eneo hilo mara moja.

Zaidi ya watu 82,000 wameondolewa Kabul, ambako wanamgambo wa Taliban wamechukua udhibiti siku 10 zilizopita.

Nchi zinanahangaika kuondoa raia wao kabla yam udo wa mwisho uliowekwa wa Agosti 31.

Image: Reuters

Maelfu ya watu bado wanasubiri ndani nan je ya uwanja huo, wakiwa na matumaini ya kuondoka nchini humo.

Taliban wamepinga kurefushwa kwa muda wa shughuli hiyolakini wameahidi kuwaruhusu raia wa kigeni na raia wa Afghanistan kuondoka nchini baada ya Agosti tarehe 31, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Siku ya Alhamis, Waziri wa Mambo ya nje wa AustraliaMarise Payne, alisema: "Kuna tisho la hali ya juu la kutokea kwa shambuio la kigaidi".

Hayo yanajiri saa kadhaa baada ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwaambia wale wanaosubiri katika lango la Abbey Gate, East Gate na North Gate "kuondoka hapo haraka iwezekanavyo".