Jamaa ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka mtoto wa mwaka mmoja

Muhtasari
  • Jamaa ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka mtoto wa mwaka mmoja
  • Watu 10 waliuawa wakati gari lililokuwa limeegeshwa nyumbani kwao lilipolipuliwa siku ya Jumapili

Mahakama moja nchini Tanzania imemuhukumu kifungo cha maisha raia mmoja wa nchi hiyo kwa kosa la kumbaka mtoto miezi 19 sawa na mwaka mmoja na miezi saba.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi nchini humo, Mahakama ya Wilaya Njombe imemkuta na hatia Steward Mkongwa (33) kupitia shauri namba 42 la mwaka 2021.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 26 mwaka 2020 katika Mtaa wa Mwembetogwa wilayani Njombe.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Isaack Mlowe alisema mshtakiwa alikiri kufanya kitendo hicho cha kumuingilia mtoto huyo baada ya mama yake kwenda kuchota maji.

Gazeti hilo limemnukuu hakimu akisema "Alifanya hivyo kwa sababu yeye alikuwa mpangaji pamoja na mama wa huyo pia alikuwa na mazoea na huyo mtoto," alisema Mlowe

Kwa habari zingine ni kuwa;

Shambulizi la droni la Marekani jumapili liliwaua watu 10 wa familia moja wakiwemo watoto 6

Shambulio lililofanywa na Marekani kutumia droni lililolenga mlipuaji wa kujitoa muhanga liliishia kuua watu 10 wa familia moja, wakiwemo watoto sita, jamaa walioponea wameiambia BBC.

Watu 10 waliuawa wakati gari lililokuwa limeegeshwa nyumbani kwao lilipolipuliwa siku ya Jumapili.

Jeshi la Marekani limesema gari lililobeba angalau mtu mmoja anayehusishwa na tawi la Afghanistan la kundi la Islamic State lililengwa.

linadokeza kuwa watu waliokuwa karibu wanaweza kuwa walishambuliwa katika tukio hilo

baadhi ya wale waliouawa hapo awali walifanya kazi na mashirika ya kimataifa na walikuwa na visa za kuwaruhusu kuingia Marekani .

Kamandi kuu ya jeshi la Marekani imesema wanachunguza ripoti za tukio hilo, lakini haijulikani ni jinsi gani watu hao 10 walifariki.

Katika taarifa, ilisema kumekuwa na idadi kubwa ya "milipuko mikubwa na yenye nguvu inayofuata" kufuatia mashambulizi ya droni’

Ilisema milipuko hiyo ilidokeza kwamba kulikuwa na "idadi kubwa ya vifaa vya kulipuka ndani, ambavyo vinaweza kusababisha majeruhi zaidi".

Kamandi hiyo hapo awali ilisema shambulio hilo lilifanikiwa "kuondoa tishio karibu" na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kabul kutoka IS-K (Dola la kiislamu -Khorasan), mshirika wa IS nchini Afghanistan.