Watu 12 wafariki DR Congo kutokana na mgodi uliovuja sumu Angola

Muhtasari
  • Watu 12 wafariki DR Congo kutokana na mgodi uliovuja sumu Angola
  • Eve Bazaiba alisema watu 12 walikuwa wamefariki dunia
  • Alisema kuwa DR Congo itauliza fidia ya uharibifu uliosababishwa lakini haikutaja kiasi
Image: BBC

Karibu watu 4,500 wameugua kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia kuvuja kwa sumu kutoka kwa mgodi wa almasi katika nchi jirani ya Angola, waziri wa mazingira anasema.

Eve Bazaiba alisema watu 12 walikuwa wamefariki dunia.

Alisema kuwa DR Congo itauliza fidia ya uharibifu uliosababishwa lakini haikutaja kiasi.

Hata hivyo, hadi kufikia hivi sasa hakuna aliyesema chchote kujibu hayo hasa kutoka kwa kampuni ya madini.

Mwezi uliopita kulikuwa na uvujaji wa kutoka eneo la uhifadhi wa bidhaa za vyuma vizito uliosababisha mto kuwa na rangi nyekundu, samaki, viboko na wanyama wengine wakafa.

Kwa habari zingine ni kuwa;

Watu sita wafariki baada ya kuingia kinyemela kwenye mgodi Burkina Faso

Wachimbaji sita haramu walifariki baada ya kuteleza kwenye mashimo ya zamani ya mgodi wa dhahabu nchini Burkina Faso.

Wengine saba walijeruhiwa paada ya polisi kurusha vitoa machozi, manusura wanasema.

Polisi walisema wachimbaji hao walikfariki kutokana na ukosefu wa oksijeni kwenye mmigodi hiyo na hawakutoa tamko lolote kuhusu utumiaji wa vitoa machozi.

Maafisa wanasema migodi iliharibiwa na magari kuteketezwa na watu wa eneo hilo baada ya tukio hilo.

Uchimbaji haramu ni kawaida nchini Burkina Faso na serikali imekuwa ikihimiza umma kushirikiana na mamlaka kuipiga vitauovu huo.