Wosia wa Mwanamfalme Philip hautawekwa hadharani kwa miaka 90

Muhtasari
  • Wosia wa Mwanamfalme Philip hautawekwa hadharani kwa miaka 90

Wosia wa mwanamfalme Philip Mtawala wa Edinburgh utasalia kuwa siri kwa miaka 90 ili kulinda "hadhi na msimamo" wa Malkia, Mahakama Kuu imeamua.

Kwa zaidi ya karne sasa imekuwa kawaida inapotokea mwanafamilia mkubwa wa familia ya kifalme akifariki, mahakama zinatakiwa kufungua na kuweka wazi wosia unaoachwa.

Uamuzi huu wa Mahakama maana yake ni kwamba, wosia wa Mwanamfalme Philip hautawekwa wazi kwa umma kama ilivyokuwa kwa wosia wa wanafamilia wengine wa familia hiyo ya kiflame.

Kutakuwa na michakato ya faragha ikiendelea katika miaka hiyo 90 kabla ya kufikiwa kwa uamuzi kuona kama wosia huo unaweza kuwekwa hadharani ama la.

Usikilizwaji wa maombi ya kufungua wosia huo ulifanyika faraghani mwezi Julai chini ya Sir Andrew McFarlane, Jaji mwandamizi wa mahakama za familia.

Alisikiliza hoja kutoka kwa mawakili wanaowakilisha upande wa mwanamfalme huyo na mwanasheria mkuu, mshauri wa kisheria wa serikali na kuchapisha uamuzi huo Alhamisi.

Mwanamfalme Philip alikuwa mtu wa aina gani?Jaji Andrew alisema kama rais wa divisheni ya familia ya mahakama kuu, yeye ndo muangalizi wa usalama wa bahasha zaidi ya 30, zilizofungwa zikiwa na wosia ulioachwa na wanafamilia wa familia ya kiflame waliofariki.

Na kwa mara ya kwaza kwa miaka zaidi ya 100, ameanzisha mchakato ambao wosia unaoachwa unaweza kuwekwa hadharani.

Sir Andrew alisema: "Nimefanya hivyo kwa sababu ya nafasi ya kikatiba, ni vizuri kuwa na utaratibu maalumu kuhusu wosia za kifalme.

"Kuna umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa maisha binafsi ya familia hii ili kuendelea kudumisha heshima ya utawala na watu wa karibu wa familia yake."

Alisema usikilizwaji wa jambo hilo ulifanywa chemba kwa lengo hilo hilo na kuongeza kuwa hakuna sababu za kisheria wakati wa usikilizwaji wake kuwakilishwa na vyombo vya habari kwa kuwa maslahi ya umma yaliwakilishwa na mwanasheria mkuuu.

Mawakili waliowakilisha upande wa mwanamfalme Philip walisema habari kuhusu maombi na usikilizwaji wa jambo hilo ungekuwa wazi ungeweza kusababaisha sintofahamu isiyouwa na msingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa malkia na familia ya kifalme.

Akitoa historia ya maamuzi yaliyopita, Sir Andrew alisema mwanafamilia wa kwanza ambaye wosia wake ulifunguliwa na Mahakama alikua Mwanamfalme Francis wa Teck, kaka yake mdogo na malkia Mary, aliyefariki mwaka 1910.

Bahasha iliyokuwa na wosia wa Mwanamfalme Francis, itakuwa kwenye usalama wa Sir Andrew, pamoja na wosia wa hivi karibuni wa mama yake na Malkia binti mfalme Margaret, ambaye ni dada yake na malkia, aliyefariki mwaka 2002.

Mwaka 2007, mtu mmoja aliyeitwa Robert Andrew Brown alijitokeza na kujitambulisha kama mtoto halali wa binti mfalme Margaret, akiomba wosia wa mama yake na malkia pamoja na binti mfalme Margaret ufunguliwe, lakini madai yake yalipingwa na kuonekana kama ya kipuuzi na kudhalilisha mchakato.

Hata hivyo Sir Andrew amerekebisha baadhi ya amri ambazo zilitaka wosia wa kifalme kutofunguliwa kwa muda usio na kikomo, na sasa zitafungulia kwa utaratibu maalumu kwa faragha baada ya miaka 90 ya uhalali wa wosia huo.

Sir Andrew alisema baada ya miaka 90 kila familia inaweza kufungua wosia kwa faragha na kupitiwa na mwanasheria wa familia ya kiflame, mtunzaji wa nyaraka za kifalme, mwanasheria mkuu na wawakilishi wowote binafsi wa mtu aliyekufa ambao wanaweza kupatikana.

Wataamua kama wosia huo unaweza kuwekwa hadharani, lakini Sir Andrew alisema baadhi ya wosia za kifalme kamwe hazitachapishwa, hata kwa sehemu ndogo tu.

Zoezi la kufungua wosia huyo zitafanywa na mtaaalam wa utunzaji wa nyaraka kuhakikisha nyaraka hizo zimetunzwa vizuri.

Masuala mengine kuhusu mchakato huo yataamuliwa na Mahakama kabla ya wosia kuanza kufunguliwa.

Mwanasheria wa Malkia na mwanasheria mkuu wa Serikali walileta hoja wakitaka wosia kutofunguliwa kwa miaka 125, lakini Jaji Sir Andrew alisema miaka 90 ni sahihi na inatosha na kwamba itamaanisha ile hatari ya kuingiliwa kwa maisha binafsi ya familia ya kiflame itakuwa imepungua.

Jaji huyo anasema anatarajiwa kuchapisha na kuweka wazi orodha yote ya majina 30 ya wosia katika bahasha anazozitunza, lakini akaongeza hatafanya hivyo mpaka kumalizika kwa mapigamizi dhidi ya uamuzi wake wa sasa, kama yatakuwepo.

Moja ya majina ambayo hayatakuwepo ni la Diana, binti mfalme wa Wales. Tofauti na wanafamilia wengine wa familia ya kifalme, wosia wake ulichapishwa baada ya kifo chake mwaka 1997, ukionyesha kwamba, mali zake nyingi ziwe kwenye mikono salama na kugaiwa kwa watoto wake watakapofikisha umri wa miaka 25.