Ni ushahidi gani uliomtia hatiani R. Kelly?

Muhtasari
  • Kwa wiki zaidi ya tano, karibu dazeni ya waathirika wa kesi ya R. Kelly walisimama mahakamani kutoa ushahidi wao kuhusu vitendo vya unyanyasaji walivyofanyiwa ya mwimbaji huyo maarufu
Image: BBC

Kwa wiki zaidi ya tano, karibu dazeni ya waathirika wa kesi ya R. Kelly walisimama mahakamani kutoa ushahidi wao kuhusu vitendo vya unyanyasaji walivyofanyiwa ya mwimbaji huyo maarufu.

Wengi kati ya wanawake na wanaume hao 11, baadhi hawawezi kuwekwa wazi kwa umma, walieleza kufanya mapenzi na R. Kelly wakiwa na umri mdogo. Wanamuelezea R. Kelly kama mtu mbabe, mwenye hasira na vurugu- wakiongeza aliwataka wamuita "baba".

Wanawake wengine wanasema walilazimika kuandika barua za usaliti, ikiwa ni pamoja na kukiri uongo ambao ungetumia baadae dhidi yao.

Septemba 27 R.Kelly alikutwa na hatia ya mashataka yaliyokuwa yakimkabili ya ulaghai na unyanyasaji wa kingono. Hukumu yake inatarajiwa kutolewa Mei 4 mwakani

Je walionyanyaswa kingono wenyewe wamesema nini kuhusu mwanamuziki huyu ambaye sasa anakabiliwa na kifungo kirefu jela?

'Nilijiokoa na kupambana'

Shahidi mmoja - aliyetambulishwa katika kesi hii ya Kelly kama Jane Doe No 5 - aliieleza mahakama kwamba R Kelly amekuwa akirejea kumnyanyasa katika uhusiano wao wa zaidi ya miaka 5, ulioanza akiwa na miaka 17 mwaka 2015.

Akiwa na miaka 23, shahidi huyo alisema pia aliambukizwa ugonjwa ulioharibu ngozi yake unaoitwa kitaalamu herpes akiwa na umri wa miaka 17 baada ya kufanya mapenzi na muimbaji huo. Anasema R. Kelly hakumfahamisha kama alikuwa na ugonjwa huo wa zinaa, kama sheria inavyotaka afanye.

"Mtu huyu alikusudia kabisa kuniambukiza ugonjwa alioujua," alisema. "Angeweza kudhibiti hali hii." Daktari wa Kelly baadae alitoa ushahidi wake kwamba muimbaji huyo alikuwa kwenye matibabu ya ugonjwa huo wa zinaa tangu 2007.

Anasema lipomfuata na kumueleza, R Kelly aligeuka mbogo na "kunieleza ningeweza kuupata ugonjwa huo kutoka kwa mtu yoyote. Nikwambia nilikuwa karibu na yeye tu ".

Image: BBC

Mwanamke mwingine aliyetambulishwa kama Faith baadaye na yeye alitoa ushahidi wake akisema aliambukizwa na Kelly ugonjwa huo wa zinaa, na mwanamke wa tatu aliyetambulishwa kama Kate alisema R Kelly alimpa dola $200,000 kama kumpooza na kumaliza mzozo baada ya kumlalamikia kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo na mwanamuziki huyo.

Akiongezea, Jane alisema Kelly alijaribu kudhibiti maisha yake na kuna wakati alimpiga mpaka kumtoa makovu.

"Nilikuwa naadhibiwa vikali karibu kila baada ya siku mbili au tatu," alisema mwanake huyo mahakamani.

Katika tukio moja, Jane anasema Kelly alimtandika kwa kutumia kiatu baada ya kugundua kuwa alimtumia meseji rafiki yake kueleza anayofanyiwa na R. Kelly. "Alinipiga kila mahali," alisema. "Nilikimbia na kupambana nae."

Jane pia alidai Kelly alimsukuma kutoa mimba yake. Na mmoja wa wasaidizi wa Kelly ndie aliyemuendesha kumpelekea Hospitali.

Jerhonda Pace

Shahidi wa kwanza, Jerhonda Johnson Pace, ameiambia mahakama kwamba R. Kelly alijua kwamba alikuwa na umri mdogo mwaka 2009 walipofanya mapenzi huko Chicago, akiwa na umri wa miaka 17.

Sasa akiwa na miaka 28, alitoa ushahidi wake katika siku ya kwanza ya kesi hiyo akisema awali alimwambia R Kelly kwamba alikuwa na miaka 19, lakini alisema umri wake sahihi siku wanafanya mapenzi na R Kelly kwa mara ya kwanza.

"Alinitaka nitengeneza nywele zangu na kuvaa kama binti skauti," baadae akaiambia mahakama kwamba, R Kelly alirekodi video wakifanya mapenzi.

Pace pia aliiambia Mahakama kwamba alikuwa anatakiwa aombe ruhusua kila anapotaka kutumia choo. "Kama hana shida na mie siku hiyo anaweza ukimuomba atatoa ruhusu ndani ya dakika moja tu, alisema lakini ikiwa hamko vizuri alikuwa analazimika kusubiri mpaka siku 3 kuruhusiwa kwenda chooni.

'Ungependa kufanya muziki?'

Watu wengine wawili walisimama kizimbani kutoa ushaidi wao kuhusu kunyanyaswa na R Kelly wakiwa sehemu ya wasaidizi wa muimbaji huyo.

Mmoja wa watu hao alitoa ushahidi wake akitumia jina la Louis, akisema alikutana kwa mara ya kwanza na Kelly mwaka 2006, wakati huo akiwa na umri wa miaka 17 akifanya kazi ya zamu ya usiku huko McDonald, Chicago.

Aliiambia Mahakama kwamba Kelly alimualika nyumbani kwake na kuna siku alimuuliza kama "angependa kufanya muziki".

Anasema alimuuliza Louis kama ameshawahi kushiriki mapenzi ya jinsia moja kabla ya kumfanyia vitendo hivyo akijua kuwa ana umri mdogo.

Baada ya hapo, "Akanambia iwe siri kati yangu na yeye", na kuongeza, "tumekuwa familia sasa, ni ndugu".

 

Mtu mwingine aliyepewa jina la Alex kwenye kesi hiyo, alisema alikutana na R Kelly kwa mara ya kwanza akiwa sekondari kabla ya kuingia kwenye uhusiano nay eye akiwa na umri wa miaka 20.

Alisema Kelly alimlazimisha kumbusu, huku akimbwambi "awe muelewa".

Baadae Kelly alikuwa akimtafutia wanawake Alex ili afanya nao mapenzi huku Kelly akiwaangalia na kuwapiga video, kuna wakati aliungana nao au aliwaangalia huku akipiga punyeto.

Alikuwa akiwaita mazombo wanawake aliofanya nao mapenzi, na alikatazwa kuzungumza na wanawake aliolala nao kimapenzi na hata kuwajua majina yao.

Kelly, alisema, alikuwa akimuita kama "mpwa", licha ya kwamba hakuwa na uhusiano wowote wa kifamilia.

'Sikutaka kuaibika'

Mwanamke mmoja ambaye alitoa ushuhuda wake kwa jina la Addie alisema alibakwa na mwanamuziki huyo huko Miami kwenye eneo ama chumba wanalotumia wanamuziki kubadilishia nguo wakati wa maonyesho "backstage'. Anasema alibakwa baada ya kumalizika kwa onyesho.

Addie alisema yeye na rafiki yake walifuatwa na wanaume wawili "walioonekana kama matunisha misuli" na kuwakaribisha 'nyuma ya jukwaa' baada ya onesho.

Walipofika, walisema Kelly aliwataka wengine kuondoka kwenye chumba hicho kabla ya kumbaka.

"Wakati huu, nilikuwa na mshangao mkubwa," aliiambia Mahakama. "Hata sikujielewa."

Baadae, rafiki yake alimwambia aripoti Polisi lakini Addie alihofia kwamba angeweza kutengwa na tasnia ya burudani kama atajitokeza kuzungumzia hilo.

"Sikujua hata kama wangeniamini," alisema. "Sikutaka kuaibika."

Binti huyo alibakwa ikiwa ni siku mbili baada ya R Kelly kutoka kumuoa binti mdogo wa wa chini ya miaka 18 aliyekuwa mwanamuziki, Aaliyah.