Wanandoa waliosambaza picha bandia za utupu za rais wa Zimbabwe waachiliwa

Muhtasari
  • Wanandoa waliosambaza picha bandia za utupu za rais wa Zimbabwe waachiliwa

Wanandoa wa Zimbabwe wameachiliwa huru kutoka kizuizini baada ya hakimu kufutilia mbali kesi dhidi yao kwa madai ya kusambaza picha bandia za utupuza rais wa taifa hilokatika mtandao wa WhatsApp, amesema wakili wao.

Sarudzayi Ambiri Jani, 39, na Remember Ncube, 35, walihukumiwa kifungo Juni 2020 kwa madai ya kuhujumuna kumtusi rais lakini hakufunguliwa mashtaka.

Picha hizo bandia zilionekana kumuonesha rais Emmerson Mnangagwaakiwa utupu , huku akiwa amezibwa na kitambaa kidogo cha bendera ya Zanu-PFna barakoa ambayo ilikuwa imeficha sehemu zake za siri.

Hakimu Takudzwa Gwazemba, aliwaachilia huru wawili hao kutoka kizuizini kwasababu upande wa mashtaka ulikuwa umeshindwa kuwafungulia mashtaka mwaka mmoja baada ya kukamatwa.

Kwingineko ni kuwa;DR Congo yaondoa marufuku ya wimbo wa kumkosoa rais

Maafisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameondoa marufuku ya wimbo unaomkosoa Rais Félix Tshisekedi.

Marufuku hiyo ilitangazwa Jumanne na tume ya udhibiti na kisha kuondolewa Jumatano baada ya waziri wa sheria kuingilia kati.

Kundi linalounga mkono muziki huo, MPR, pia lilisema limeomba marufuku hiyo kuondolewa.

Marufuku hiyo ilikuwa imeonekana kuwa ya kidikteta na ilikosolewa sana.

Vyombo vya habari sasa vimeruhusiwa kupiga wimbo Nini Tosali Te (Nini Hatukufanya katika lugha ya Kilingala). Wimbo huo unalinganisha kile ambacho Bw Tshisekedi aliahidi alipokuwa kwenye upinzani na kile ambacho amefanikiwa kufikia sasa akiwa rais.

"Ulituahidi furaha baada ya [marehemu rais] Mobutu kuondoka. Mobutu alienda lakini hatukupata chochote. Ulisema ungerekebisha mambo ikiwa [rais wa zamani] Kabila atajiuzulu. Kabila aliondoka lakini bado ni ngumu," AFP. shirika la habari linanukuu maneno hayo yakisema.

Wimbo mwingine mmoja katika Kifaransa, Barua kwa Ya Tshitshi, jina la utani la marehemu babake Bw Tshisekedi, Etienne, bado umepigwa marufuku.

Mwimbaji, Bob Elvis, anasema: "Tangu uondoke, mwanao Felix amekuwa rais... Tumebadilisha utawala bila kubadilisha mfumo," AFP inaripoti.

Msemaji wa serikali Patrick Muyaya alitweet kwamba marufuku hiyo haikutoka kwa serikali.

“Mwananchi yeyote ana uhuru wa kutoa maoni yake, mradi yanazingatia sheria,” alisema.

Idadi ya kutazamwa kwa nyimbo hizo mbili imeongezeka kwenye YouTube tangu kupigwa marufuku, kulingana na tovuti ya habari ya Actualite Congo.