- Makumi wapatikana na virusi katika ndege iliyotoka Afrika kusini kwenda Uholanzi
- Wamewekwa katika eneo la kujitenga katika hospitali iliyopo karibu na uwanja wa ndege wa Schiphol
Watu sitini na mmoja waliowasili mjini Amsterdam katika ndege mbili zilizotoka Afrika Kusini wamepatikana na virusi Covid-19, Dwamesema maafisa wa Uholanzi.
Wamewekwa katika eneo la kujitenga katika hospitali iliyopo karibu na uwanja wa ndege wa Schiphol.
Walikuwa ni miongoni mwa wasafiri wapatao 600 walikuwa wameshikiliwa kwa saa kadhaa baada ya kuwasili huku wakipimwa virusi.
Maafisa wa Uhonzi wanafanya vipimo zaidi kuangalia iwapo kuna visa vovyote vya kirusi kipya cha Omicron, kilichopewa jina hilo Ijumaa, kilichotajwa kama aina mpya ya kuhofia na WHO.
Aina hiyo mpya ya kirusi cha covid kwa mara ya kwanza kiliripotiwa kwa Shirika la afya duniani nchini Afrika Kusini tarehe 24 Disemba.
Wakati huo huo Uholanzi ni mojawapo yan chi kadhaa za Muungano wa Ulaya zinazohangaika kudhibiti rekodi ya idadi ya maambukizi.
Katika kipindi cha saa kadhaa nchi nyingi kote duniani zimeweka masharti ya kusafiri kutoka katika nchi za kusini mwa Afrika zilizoathiriwa.
Nini tunachokifahamu mpaka sasa kuhusu Kirusi hicho?
Kirusi hicho kinaitwa B.1.1.529 na huenda Ijumaa hii Shirika la Afya Duniani (WHO) likakipa kirusi hicho jina la Kigiriki (kama lilivyo kwa kirusi cha Alpha na Delta).
Prof Tulio de Oliveira, mkurugenzi wa Kituo cha Kukabiliana na Magonjwa ya mlipuko nchini Afrika Kusini, alisema kulikuwa na "mfululizo usio wa kawaida wa mabadiliko" na kwamba ilikuwa "tofauti sana" na tofauti aina zingine za virusi ambazo zimeenea.
"Aina hiki cha kirusi kilitushangaza, kina mabadiliko mengi zaidi kuliko ambavyo tulitarajia," alisema.
Profesa Richard Lessells, kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini, alisema: "Tunapata wasiwasi kwamba virusi hivi vinaweza kujiimarisha, na kuimarisha uwezo wake kuenea kutoka kwa mtu hadi mtu, lakini pia kinaweza kuepuka mfumo wa kinga."
Athari zake zikoje mpaka sasa?
Bado ni mapema kutoa hitimisho la wazi kuhusu athari, lakini tayari kuna ishara ambazo zinaleta wasiwasi.
Kumekuwa na visa 77 vilivyothibitishwa katika jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini, visa vinne nchini Botswana na kimoja Hong Kong (ambavyo vinahusishwa moja kwa moja na watu kusafiri kutoka Afrika Kusini).
Kuna matokeo ya haraka yanaweza kupatikana katika vipimo vya kawaida na ambayo inaweza kutumika kufuatilia kirusi hiki bila kufanya uchambuzi kamili wa maumbile.
Kwa hivyo kwa sasa tumeachwa na virusi vinavyoleta wasiwasi kubwa licha ya uelewa wetu mdogo kuvihusu, na ni moja ambayo inahitaji kuangaliwa kwa karibu na kuuliza maswali ya kina juu ya nini cha kufanya na wakati gani. Somo la janga ni huwezi kusubiri kila wakati mpaka uwe na majibu yote.
Hiyo inaonyesha 90% ya visa katika jimbo la Gauteng vinaweza kuwa tayari vimeshamiri na "inaweza kuwa tayari kuwepo katika maeneo mengine" nchini Afrika Kusini.
Lakini hii haituambii ikiwa kinaenea kwa kasi zaidi kuliko kirusi cha Delta, ni kikali zaidi au kwa kiwango gani inaweza kuepuka kinga ya kinga inayotokana na chanjo.
Pia haituambii ni kwa kiasi gani tofauti kitaenea katika nchi zilizo na viwango vya juu zaidi vya chanjo kuliko asilimia 24 ya Afrika Kusini, ingawa idadi kubwa ya watu nchini humo wamekuwa na maambukizi ya Covid.
Kwa sasa tumebaki na wasiwasi mkubwa kuhusu kirusi hiki, licha ya uelewa mdogo kuvihusu, ni moja ya virusi vinavyopaswa kuangaliwa na kufuatiliwa kwa karibu na kuuliza maswali ya kina juu ya nini cha kufanya na wakati gani. Somo kubwa kuhusu janga la corona ni kwamba huwezi kusubiri mpaka uwe na majibu yote.