Je ni kwa nini wakfu wa Mwanamitindo Naomi Campbell unachunguzwa?

Muhtasari
  • Mwaka 2005, Campbell alianzisha wakfu ili kuchangisha fedha za Watoto wanaoishi katika hali ya umasikini na mazingira mabaya
  • Wakfu huo unasema kwamba umachangisha mamilioni ya paundi ili kutumia katika mipango ya hisani
Naomi Campbell
Image: BBC

Wakfu wa fesheni ulioanzishwa na mwanamitindo maarufu wa Uingereza Naomi Campbell umesema kwamba unashirikiana na wachunguzi kuhusu malalamishi ya usimamizi mbaya na fedha zake.

Mwaka 2005, Campbell alianzisha wakfu ili kuchangisha fedha za Watoto wanaoishi katika hali ya umasikini na mazingira mabaya.

Wakfu huo unasema kwamba umachangisha mamilioni ya paundi ili kutumia katika mipango ya hisani.

Tume ya mashirika ya hisani , ambayo inadhibiti kazi ya mashirika hayo nchini England imesema kwamba wakfu huo wa Campbell awali ulikuwa ukichunguzwa kutokana na ukiukaji wa sheria zake.

Wakati wa kesi hiyo, ilioanzwa Septemba 2020, tume hiyo ilibaini baadhi ya malalamishi kuhusiana na usimamizi wa shirika hilo na fedha zake.

''Hii ni pamoja na shirika la usaidizi kuchelewa kuwasilisha taarifa za akaunti mara kwa mara na ukosefu wa ushahidi kwamba migongano ya kimaslahi ilikuwa ikishughulikiwa'', tume ilisema.

Mnamo Machi mwaka huu, UNHCR ilitayarisha mpango kazi kwa wadhamini unaolenga kuboresha usimamizi wa fedha wa shirika hilo la hisani

Baada ya kukagua majibu ya mpango kazi wa shirika hilo , wadhibiti walitambua baadhi ya maeneo yanayotiliwa shaka na jinsi usimamizi wa fedha wa shirika hilo ulivyofanywa.

Kutokana nah atua hiyo kamati inayosimaia mashirikma ya hisani ilitaka uchunguzi wa wazi kufanywa.

Iwapo wale wanaosimamia wakfu huo wamefuata sheria chini ya kifungo cha sheria za wakfu pia itajulikana.

Ama iwapo kumekuwa na utovu wa nidhamu na/au usimamizi mbaya miongoni mwa wale wanaosimamia shirika hilo la misaada.

Msemaji wa taasisi hiyo alisema katika taarifa yake kwamba inatumai "kukomesha ushirikiano na shirika la UNHCR haraka iwezekanavyo," akiongeza kuwa taasisi hiyo imeomba kuongezwa kwa muda huo kwa sababu haikuweza kufanya shughuli zozote za uchangishaji fedha kwa miaka miwili kutokana na jangwa la corona duniani.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa "dokezo lolote la makosa au utovu wa nidhamu wa wadhamini ni uwongo."

Alisema kuwa Fashion Relief sio tu shirika la msaada wa kuchangisha pesa, bali pia limeandaa hafla za kusaidia kuhamasisha michango kwa misaada mingine.

"Hafla zote hufanyika kwa manufaa ya wafadhili wengine. Katika kila hafla, michango na ahadi zote hutolewa moja kwa moja kwa mashirika hayo ," taarifa hiyo ilisoma.