Tamasha la Koffi Olomide kufanyika Rwanda, licha ya kilio cha wanaharakati

Muhtasari
  • Bado kuna watu wengi wanaoendelea kupinga tamasha la muziki la Koffi Olomide kufanyika mjini Kigali kufuatia kupatikana na hatia ya unyanyasaji dhidi ya wanawake 
koffi
koffi

Kampuni iliyoandaa tamasha la muziki la mwanamuziki wa DRC Koffi Olomide mjini Kigali imesema kuwa haina muda wa kuzungumzia kuhusu mashitaka yanayomkabili mwanamuziki huyo, na badala yake inaahidi kuwa kutakuwa na onyesho’’tamu ‘’ Jumamosi ijayo.

Bado kuna watu wengi wanaoendelea kupinga tamasha la muziki la Koffi Olomide kufanyika mjini Kigali kufuatia kupatikana na hatia ya unyanyasaji dhidi ya wanawake .

Bruce Intore, mkuu wa kampuni iliyoandaa tamasha hilo- Intore Entertainment, amefafanua "suala hilo litatatuliwa na ngazi husika ikiwa ni pamoja na mahakama ".

Bw Bruce Intore amesema "tunaheshimu mawazo na haki za watu wenye wenye maoni tofauti kumuhusu msanii huyu."

Watu wapatao 1200 tayari wamekwisha saini la kutaka tamasha la Koffi olomide analotarajia kulifanya mjini Kigali lisitishwe.

Mahakama ya Paris Ufaransa inatarajiwa kutoa hukumu mwaadaye mwezi huu kuhusiana na mashitaka ya wanenguaji wa zamani wa Koffi Olomide ya ubakaji.

Wiki iliyopita mwanaharakati wa hai za wanawake nchini Rwanda Juliette Karitanyi, aliiambia BBC kuwa: "Kumruhusu [Koffi Olomide] kufanya tamasha hapa, ni sawa na kuwapuuza wale aliowanyanyasha .

KWINGINEKO NI KUWA;

Miili 9 zaidi yapatikana baada ya tukio la kuzama kwa boti Nigeria

Maafisa wa Nigeria wamethibitisha kuwa miili tisa zaidi ya mkasa wa ajali ya boti ya Jumanne imepatikana Jumatano asubuhi.

Hii inafanya idadi ya waliofariki kufikia 29 kufikia sasa.

Shughuli ya utafutaji na uokoaji inaendelea ikihusisha polisi, zima moto na wanachama wa Kikosi cha Usalama na Ulinzi wa Raia wa Nigeria pamoja na waliojitolea.

Polisi katika eneo hilo wameiambia BBC kwamba idadi ya manusura waliookolewa kufikia sasa bado ni saba.

Manusura wa ajali ya boti walikuwa wengi wanafunzi wa shule ya Kiislamu - wenye umri wa kati ya miaka sita na 12 - waliokuwa wakisafiri kwenda kwenye sherehe za kidini katika mji wa Bagwai.