Rais Samia afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kubuni wizara mpya

Muhtasari
  • Rais Samia afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kubuni wizara mpya
Image: IKULU

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kubuni wizara mpya.

Akitangaza mabadiliko hayo , Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo ikiwa anatimiza ahadi yake ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Kulingana na mabadiliko hayo Wizara ya katiba na sheria imepata waziri mpya George Simbachawene ambaye amechukua wadhifa wa Profesa Palamagamba Kabudi.

Wizara ya Habari na teknolojia ya habari pia itaongozwa na Waziri mpya aliyekuwa Waziri wa zamani Nape Nnauye.

Mengi yafuata;