Mwanamume wa Marekani apandikiziwa moyo wa nguruwe katika upasuaji wa mara kwanza duniani

Muhtasari

• Madaktari wa Chuo Kikuu cha Maryland kito cha tiba walipewa idhini maalum na wasimamizi wa matibabu kuendelea na upasuaji huo, kwa misingi kwamba vinginevyo Bw Bennet angekufa.

• David Bennett, mwenye umri wa miaka 57, anaendelea vyema siku tatu baada ya upasuaji wa majaribio hayo uliofanyika katika mji wa Baltimore, wanasema madaktari.

• Mwezi Oktoba, 2021, madaktari wa upasuaji mjini New York walitangaza kwamba wamefanikiwa kupandikiza figo la nguruwe kwa binadamu.

Daktari wa upasuaji kwa jina Bartley P. Griffith akiwa pichani na David Bennett mapema mwezi huu.
Daktari wa upasuaji kwa jina Bartley P. Griffith akiwa pichani na David Bennett mapema mwezi huu.
Image: UNIVERSITY OF MARYLAND SCHOOL OF MEDICINE

Mwanaume wa marekani amekuwa mtu wa kwanza kabisa duniani kupata moyo wa nguruwe aliyebadilishwa vinasaba(GMO).

David Bennett, mwenye umri wa miaka 57, anaendelea vyema siku tatu baada ya upasuaji wa majaribio hayo uliofanyika katika mji wa Baltimore, wanasema madaktari.

Upandikizaji wa moyo huo unachukuliwa kama matumaini ya kuyaokoa maisha a Bw Bennett, ingawa haijawa wazi bado ni fursa ya kiasi gani aliyo nayo ya kuishi maisha marefu.

" Ulikuwa ni upandikizaji wa kufanya au afe," Bw Bennett alielezea siku moja kabla ya upasuaji.

''Ninafahamu kwamba ni jambo la kubahatisha, lakini ni chaguo langu la mwisho," alisema.

Madaktari wa Chuo Kikuu cha Maryland kito cha tiba walipewa idhini maalum na wasimamizi wa matibabu kuendelea na upasuaji huo, kwa misingi kwamba vinginevyo Bw Bennet angekufa.

Alikuwa ameonekana kwamba hakuwa na uwezo wa kupandikiziwa moyo wa binadamu, uamuazi ambao mara nyingi huchukuliwa na madaktari wakati mgonjwa anapokuwa na afya duni sana.

Kwa timu ya madaktari iliyofanya upandikizaji huo, mafanikio hayo yamehitimisha miaka kadhaa ya utrafiri na yanaweza kubadili maisha kote duniani.

Daktari wa upasuaji Bartley Griffith alisema upasuaji utaileta dunia katika "hatua moja ya kukaribia kutatua mzozo wa ukosefu wa kiungo cha mwili ",Chuo kikuu cha tiba cha Maryland kilisema katika taarifa yake kwa umma.

Kwamba mzozo huo unamaanisha kuwa watu 17 kwa siku hufariki nchini Marekani wakati wakisubiri kufanyiwa upasuaji wa kupandikiziwa viungo, huku zaidi ya 100,000 wakiripotiwa kungojea upasuaji.

Uwezekano wa kutumia viungo vya Wanyama kwa ajili ya kile kinachoitwa xenotransplantation ili kufikia mahitaji umekuwa ukifikiriwa kwa muda mrefu, na matumizi ya mishipa ya moyo wa nguruwe tayari limekuwa ni jambo la kawaida.

Mwezi Oktoba, 2021, madaktari wa upasuaji mjini New York walitangaza kwamba wamefanikiwa kupandikiza figo la nguruwe kwa binadamu.

Wakati huo, upasuaji huo ulikuwa ni jaribio la teknolojia ya hali ya juu zaidi kuwahi kufikiwa.

Hatahivyo, ubongo wa mtu alyepandikiziwa ulikufa na hakuna matumaini ya kupona.

Upasuaji huo, uliofanyika katika Baltimore, Maryland, ulichukua muda wa zaidi ya saa saba kukamilika
Upasuaji huo, uliofanyika katika Baltimore, Maryland, ulichukua muda wa zaidi ya saa saba kukamilika
Image: UNIVERSITY OF MARYLAND SCHOOL OF MEDICINE

Bw Bennett, hatahivyo , anamatumaini kuwa upandikizaji wake wa moyo wa nguruwe utamuwezesha kuendelea na maisha yake.

Alikuwa amelala kitandani kwa wiki sita mfulurizo kabla ya kufanyiwa upasuaji, na aliwekewa mashine ambayo ilimuwezesha kuendelea kuishi baada ya kupatikana na maradhi yanayoua ya moyo.

"Natazamia kunyenyuka na kuondoka kitandani baada ya kupona ," alisema wiki iliyopita.

Jumatatu, Bw Bennett aliripotiwa kupumua mwenyewe huku akiendelea kufuatiliwa kwa karibu.

Lakini kile kitakachotokea baadaye hakijawa wazi. Nguruwe aliyetumiwa katika upandikizaji alifanyiwa mabadiliko ya vinasaba ili kuondoa jeni kadhaa ambazo zingefanya kiungo hicho kikataliwe na mwili wa Bw Bennet, linaripoti shirika la habari la AFP.

Bw Griffith anasema wanaendelea kumfuatilia kwa makini na kwa uangalifu mkubwa, huku mwanae wa kiume David Bennett Jr akiliambia Shirika la Habari la ovAssociated Press kwamba familia yao iko "katika hali ya sintofamu wakati huu".

Lakini aliongeza : "Alitambua ukubwa wa kile kilichofanyika na anatambua umuhimu wake."

''Hatujawahi kufanya hili kwa binadamu na ninapenda kufikiria kwamba tumempatia chaguo bora kuliko kile ambacho kingetokea kama angeendelea kupewa matibabu aliyokuwa akiyapata," alisema Bw Griffith . Lakini iwapo [ataishi kwa] siku, wiki , mwezi, au mwaka, sijui."