Wanahabari 6 miongoni mwa watu 14 waliofariki katika ajali Tanzania

Muhtasari

• Wanahabari sita ni miongoni mwa watu 14 waliofariki mapema siku ya Jumanne katika ajali ya barabarani nchini Tanzania.

Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Image: GOOGLE

Wanahabari sita ni miongoni mwa watu 14 waliofariki mapema siku ya Jumanne katika ajali ya barabarani nchini Tanzania.

Ajali hiyo ilitokea wakati gari la waandishi wa habari lililokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel kugongana na gari moja la abiria katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda alizuru hospitali ambako majeruhi walipelekwa na kuahidi kutoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel pia alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametuma risala zake za rambi rambi kwa jamaa za waliofiwa.

Kupitia ujumbe aliotundika kwenye Twitter rais Samia alisema alishtushwa na vifo vya 14 hao.